Saturday, November 28, 2020

OSCAR NYOTA MWINGINE ALIYENASA KWENYE MTEGO WA FEDHA ZA WACHINA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

HATIMAYE klabu za Ligi Kuu China zimeendeleza kufuru yao ya fedha kwenye ulimwengu wa soka.

Hivi karibuni taarifa iliyoteka vichwa vingi vya habari ni ile ya Chelsea kukubali ofa ya pauni milioni 60 kumuuza staa wao Oscar kwenda kujiunga na Shanghai SIPG.

Licha ya umri mdogo wa miaka 25 alionao, Mbrazil huyo anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo wakati wa dirisha dogo la usajili la Januari.

Hata hivyo, kuna maswali ambayo kila shabiki wa soka angekuwa anajiuliza kufuatia uhamisho huo wa fedha nyingi  kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 25.

Kwanini  Oscar amekwenda China?

Sababu kubwa inayoonekana kwa nyota huyo kukubali uhamisho huo ni fedha. Kwanza, kiasi alichonunuliwa cha pauni milioni 60, kimeipa faida kubwa Chelsea.

Kutokana na dili hilo, Cheslea wamepata faida ya pauni milioni 35 kwani wao walipomnunua mwaka 2012 walitumia pauni milioni 25 tu. Haikuwa rahisi kwa Chelsea kukataa ofa hiyo.

Lakini pia, kukubali kuchezea Shanghai kunampa Oscar uhakika wa kuingiza mshahara mnono wa pauni 400,000 kwa wiki.

Sababu nyingine ni kukosa namba ya uhakika kwenye kikosi cha Antonio Conte.

Ameingia kwenye kikosi cha kwanza mara tano pekee na ametokea benchi katika mechi nne.

Kuna uwezekano mkubwa wa kuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi cha Shanghai.

Atakutana na mastaa gani Shanghai SIPG?

Kwanaza, atafanya kazi chini ya kocha wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas. Villas-Boas alichukua mikoba hiyo baada ya Sven-Goran Eriksson kutimkia Shenzhen FC.

Atacheza na Mbrazil mwenzake Hulk ambaye ndiye straika wa timu hiyo.

Wengine atakaocheza nao kikosini ni Dario Conca, Jean Evrard Kouassi, Ju-Young Kim, Yan Junling, Fu Huan, Sun Xiang, Yu Hai, Cai Huikang na Wu Lei.

Shanghai SIPG inapata wapi fedha?

Matanuzi makubwa ya Shanghai SIPG yanatokana na fedha nyingi inazopata kutoka kampuni yao inayoendesha bandari ya jijini Shanghai. Ni moja kati ya kampuni kubwa China na Serikali ya Shanghai inamiliki asilimia 61 ya hisa zake.

Oscar atavaana na mastaa gani?

Miongoni mwa timu atakazokutana nazo ni Guangzhou Evergrande inayonolewa na Luiz Felipe Scolari ambaye aliipa ubingwa wa mwaka huu. Staa wa zamani wa Tottenham, Paulinho na mpachikaji mabao wa zamani wa Atletico Madrid, Jackson Martinez, naye wanakipiga Guangzhou.

Pia, Oscar atakuwa akivaana na Demba Ba (Shanghai Shenhua), Ramires (Jiangsu Suning) na Gael Kakuta (Hebei China Fortune),  Obafemi Martins (Shenhua) na Papiss Cisse (Shandong Luneng) na Graziano Pelle anayekipiga katika klabu ya Shandong Luneng.

Wachezaji gani wanaweza kumfuata Oscar China?

Bado klabu za China zimeendelea kutishia kuviteka vipaji vya soka vya barani Ulaya na kwingineko duniani.

Mmoja wao ni Tevez ambaye pia ameahidiwa dau nono ikiwa atakubali kutua China.

Lakini pia, orodha hiyo inawajumuisha John Terry, Wayne Rooney na Alexis Sanchez. Hivi sasa, hali si shwari katika klabu ya Arsenal ambapo staa Sanchez ambaye amekuwa tegemeo katika siku za hivi karibuni, amegoma kutosaini mkataba mpya akishinikiza maboresho ya malipo yake.

Kutokana na umri, huenda hata Terry akashindwa kupuuzia fedha za China, kitu ambacho pia kinaweza kufanywa na Rooney ambaye amekuwa akitajwa kwenye mpango huo kwa misimu kadhaa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -