Tuesday, October 20, 2020

Owino aipa Stand United nafasi ya Simba

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA ZAINAB IDDY

BEKI wa zamani wa Simba na Timu ya Taifa ya Uganda, Joseph Owino, ameitabiria makubwa Stand United, baada ya kusema timu hiyo ina nafasi ya kumaliza msimu ikiwa kwenye nafasi ya tatu.

Beki huyo kwa sasa anaichezea timu ya Fanja FC, inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Oman.

Kabla ya kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Fanja FC, Owino aliitumikia Stand United kwa kipindi kifupi katika Ligi Kuu inayoendelea.

Akizungumza na BINGWA, Owino amesema licha ya mgogoro uliopo katika klabu hiyo ukihusisha pande mbili zinazopingana, bado timu hiyo inaweza kufanya makubwa msimu huu kutokana na ubora ilionao.

“Ukiondoa mgogoro uliopo ndani ya timu, Stand wana kikosi bora ambacho kina uwezo wa kumaliza ligi kikiwa katika nafasi   za juu kama nafasi ya tatu.

“Kikubwa ni wachezaji kujua majukumu yao na kuacha kusikiliza migogoro ya kiuongozi ambayo haina faida kwao, wao wanatakiwa kufanya kazi yao ambayo ni kucheza mpira na kuipa matokeo,” alisema Owino.

“Naamini hilo likifanyika timu ina nafasi ya kumaliza katika nafasi ya tatu.”

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Stand United ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 15, nyuma ya Simba inayoongoza ikiwa na pointi 17.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -