Saturday, October 31, 2020

OZIL, SANCHEZ BADO, GIROUD, COQUELIN WAONGEZA MKATABA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

WAKATI mashabiki wa Arsenal wakisubiri kusikia Habari nzuri za kuongezwa mkataba kwa nyota wao, Mesut Ozil na Alexis Sanchez, nyota hao bado wameweka ngumu.

Lakini wakati wawili hao wakiwa bado hawajaamua kuongeza mikataba yao,  Washika bunduki hao wa jiji la Londol wamefanikiwa kuwaongezea mkataba mpya wachezaji wao, Laurent Koscielny, Olivier Giroud na Francis Coquelin.

Gunners walikuwa kwenye mazungumzo na wachezaji wao hao muhimu kwa miezi kadhaa na sasa wote wameongeza mkataba mpya.

Wachezaji hao watatu walikuwa wamebakiza miezi 18 kwenye mikataba yao ya zamani, hivyo mashabiki wa Arsenal watakuwa na matumani kwamba ni mwanzo mzuri kwa wachezaji kama Sanchez na Ozil kuongeza mikataba yao.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, alisema: “Tumefurahi kwamba wachezaji wetu muhimu watatu wameongeza mkataba mpya.

“Ameonyesha ufundi mkubwa katika miaka ya hivi karibuni kwa kuwa yuko makini. Olivier ana uzoefu mkubwa kwenye mechi na amekuwa mchezaji kamili tangu alipojiunga na sisi. Laurent naye ni mchezaji muhimu kikosini na anaamini ni mmoja kati ya mabeki bora duniani kwa sasa. Hivyo kiujumla hizi ni habari njema.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -