Monday, November 23, 2020

‘Ozil si wa sayari hii’

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Arsenal na mchambuzi wa Sky Sports, Charlie Nicholas, ameshindwa kumwelezea kiungo Mesut Ozil na kusema ‘anatoka sayari nyingine’, baada ya bao lake kali alilotumia juhudi binafsi na kuisaidia timu yake ya Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ludogorets na kuivusha Gunners hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kikosi hicho cha Arsene Wenger ambacho kiliifunga klabu hiyo ya Bulgaria mabao 6-0 kwenye mechi ya kwanza, walihitaji kutoka nyuma kwa mabao 2-0 dhidi ya Ludogorets kabla ya Ozil kuwahakikishia ushindi wa pointi zote tatu dakika ya 87 kwenye mchezo wa juzi Jumanne.

Kiungo wa Misri aliyeingia akitokea benchi, Mohamed Elneny, alimpigia pasi ndefu nyota huyo wa Ujerumani, ambaye alimpiga kanzu mlinda mlango wa Ludogorets na kuwapiga chenga mabeki wawili na kufunga bao hilo.

Mchambuzi huyo wa Sky Sports, Nicholas ambaye alikuwa akifuatilia mechi hiyo, alimsifia nyota huyo mwenye umri wa miaka 28.

“Ozil yuko kwenye kiwango cha kipekee,”  Nicholas alizungumza kwenye Sky Sports. “Anatoka kwenye sayari nyingine ambayo hakuna mchezaji wa Arsenal ambaye amefika.

“Ana kipaji bab kubwa na anajua namna ya kuwakimbia mabeki. Ozil alicheza vizuri sana.”

Nicholas aliongeza: “Alionyesha kile alichofanya dhidi ya Chelsea baada ya kukimbia na mpira kwa umbali mrefu na kushirikiana na Alexis Sanchez na kufunga bao.”

“Mwishoni mwa wiki hii watacheza dhidi ya Spurs, kisha baada ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa wataenda Old Trafford. Hizo ni mechi ambazo wanapaswa kushinda ambapo wachezaji kama Ozil wanapaswa kuonekana kwenye matukio kama hayo.”

Arsenal walikuwa wamekwishafungwa mabao 2-0 ndani ya dakika 15, baada ya mabao ya Jonathan Cafu dakika ya 12 na dakika tatu baadaye Claudiu Keseru alifunga jingine, lakini walipambana na mabao ya Granit Xhaka na Olivier Giroud yaliwafanya kwenda mapumziko wakiwa sawa kwa mabao 2-2.

Kisha walitafuta nafasi ya kuibuka na ushindi dakika za majeruhi, ambapo juhudi binafsi za Ozil ziliisaidia Arsenal kupata ushindi na kutinga 16 bora ya michuano hiyo kwa miaka 17 mfululizo na Nicholas kusema kwamba Gunners wanazidi kuwa ‘mcharo’ msimu huu.

“Kiujumla ni timu ambayo mwaka mmoja uliopita, ungeweza kuionea huruma na kusema bahati haikuwa yao,” alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal.

“Walibanwa na Sunderland ambao walifanya matokeo kuwa 1-1 kabla ya kushinda mabao 4-1, huku wakipigwa 2-0 kwenye mchezo wa Jumanne na baadaye kusawazisha na kuibuka na ushindi, hayo ni mabadiliko makubwa kutokea Arsenal.

“Nafikiri kwa wachezaji waliomo kwenye kikosi, kurejea kwa Aaron Ramsey na Olivier Giroud, timu inazidi kupata nguvu.”

Kutokana na kuwa na mchezo ‘London derby’ dhidi ya Tottenham, Arsenal walifanya mabadiliko ya wachezaji watano kutoka kikosi kile kilichoifunga Sunderland mwishoni mwa wiki, ambapo Theo Walcott, Hector Bellerin, Santi Cazorla na Nacho Monreal wote hawakucheza mechi ya juzi nchini Bulgaria.

Lucas Perez, Per Mertesacker na Danny Welbeck ndio wachezaji ambao watakuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeruhi, lakini kikosi hicho cha Arsenal kilionyesha kwamba kina wachezaji wa kutosha baada ya Ramsey na Giroud kuanza kwenye mechi hiyo ya Jumanne.

“Arsenal sasa hivi wako vizuri,”  alisema Nicholas. “Ozil yuko moto, yeye na Sanchez wanacheza vizuri pamoja, umempata mpambanaji Giroud.

“(Theo) Walcott anapambana na (Alex) Oxlade-Chamberlain anataka nafasi, huku Ramsey amerejea.

“Ukiangalia benchi la Barcelona, Real Madrid na Atletico hawana kikosi kipana ambacho wanacho Arsenal, je, wataweza kuungana pamoja na kufanya kweli? Huu ndio wakati wao?”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -