LAGOS, Nigeria
BAADA ya mfarakano wa miezi kadhaa kati ya wanandugu, Peter na Paul ambao wanaunda kundi la P-Square sasa unaweza kusema ‘bifu’ hilo halipo tena.
Hii ni kutokana na kwamba vinara hao wamefyatua wimbo mpya walioupa jina la Bank Alert.
Kabla ya kufyatua kibao hicho wanandugu hao wazaliwa wa familia ya Okoye, bifu lao hilo lilianza baada ya Peter Okoye kumtimua Jude katika nafasi ya umeneja hali ambayo ilisababisha kuwapo na maswali mengi katika mitandao ya kijamii.
Bifu hilo lilishika kasi zaidi wakati Peter alipotishia kumfungulia mashtaka kaka yake, Paul Okoye, kwa kufanya tamasha nchini Congo peke yake huku akitumia jina na kundi lao.
Hata hivyo, baadaye kama wasemavyo wahenga, ndugu wakigombana chukua jembe ukalime wakipatana chukua panga ukavune ndivyo ilivyokuwa kwa nyota hao baada ya kufarakana waliamua kuweka tofauti zao kando na sasa wanapiga mzigo kwa kwenda mbele.