Tuesday, December 1, 2020

PAMBANO LA WATANI… WATATU YANGA CHINI YA ULINZI

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

HUSSEIN OMAR NA EZEKIEL TENDWA,

MECHI zinazowakutanisha mahasimu Simba na Yanga, zina mambo yake asikwambie mtu kama inavyojionyesha kwa sasa kuelekea pambano la kukata na shoka baina ya wakongwe hao mwishoni mwa wiki hii.

Wakati watani hao wa jadi wakitarajiwa kuvaana Jumamosi katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, tayari tambo zimeanza kwa pande zote mbili, kila mmoja akikifagilia kikosi chake kuwa na nafasi kubwa ya kushinda.

Utamu wa mchezo huo umeonekana kukolezwa zaidi na mbio za ubingwa kwani timu hizo zinafukuzana kileleni kiasi kwamba itakayoshinda Jumamosi ndiyo itakayokuwa na nafasi kubwa ya kubeba kombe.

Lakini wakati mashabiki na viongozi wakionekana kuwa na hamasa kubwa na mchezo huo, kwa baadhi ya wachezaji imekuwa tofauti kwao kwani mara kwa mara wamejikuta wakikabiliwa na vishawishi vya fedha nyingi kutoka kwa timu pinzani wakishinikizwa kucheza chini ya kiwango au kufungisha ili kuubeba upande fulani.

Kwa kufahamu hilo, safari hii Yanga wamejipanga kuhakikisha wanaziba mwanya huo ili kutimiza azma yao ya kushinda na kujiweka katika mazingira mazuri ya kulibakiza kombe Jangwani wakiwa kama mabingwa watetezi.

Katika mkakati wao huo, Yanga wameandaa mpango maalumu wa kufuatilia mawasiliano pamoja na uchezaji wa kila mchezaji wao, kuanzia dakika ya kwanza hadi ya 90 kuona kama yupo atakayefanya uzembe wowote wa makusudi ili kuihujumu timu yao.

Habari kutoka ndani ya Yanga, zinasema kuwa miongoni mwa mbinu watakazozitumia ni kupandikiza watu ndani ya Simba wenye uwezo wa kupata taarifa zozote za wachezaji wao waliotumiwa na watani wao hao, lakini pia kuwarekodi kwa video wachezaji wao nyota ili mwisho wa siku waweze kupitia video hizo kuona kama kuna aliyewahujumu wajue la kufanya.

Mmoja wa viongozi wa Kamati ya Mashindano ya Yanga ambaye amekataa jina lake kuwekwa hadharani, ameliambia BINGWA: “Tunajua watani zetu huwa wana mbinu nyingi za kimchezo na wapo ambao ni mabingwa wa kuhujumu wachezaji, sasa hilo safari hii tumeamua kulivalia njuga na mchezaji atakayekubali kurubuniwa atakiona cha moto.”

Alipoulizwa mbinu watakazozitumia alijibu: “Zipo nyingi…tutawarekodi kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo hadi mwisho, lakini pia tutafuatilia mawasiliano yao yote. Mchezaji atakayebainika kuihujumu timu, tutamshtaki kwa mashabiki na wanachama wetu ili wajue adhabu gani ya kumpa, lakini pia kama viongozi, tutakutana tujue cha kufanya.”

Kwa bahati mbaya, mipango hiyo ya Yanga inakuja wakati timu hiyo ikiwa katika wakati mgumu kwani iwapo itafungwa na Simba, inaweza kujikuta ikilikodolea macho kombe likihamia Mtaa wa Msimbazi.

Lakini pia, mashabiki wa Yanga kwa sasa wanaonekana kuwa katika wakati mgumu kutokana na tambo za wenzao wa Simba ambao kwa siku za hivi karibuni wamekuwa wakiwakejeli kwa nyimbo kede kede za dhihaka kiasi cha kuwakosesha raha Wanajangwani hao.

Kutokana na hali hiyo, watu wa Yanga wanaamini dawa pekee ya kuwanyamazisha Simba ni kuwapiga mabao mengi tu, tena ikiwezekana kuanza kuzitikisa nyavu zao dakika ya kwanza tu ya mchezo ili kuzizima nyimbo zao za kejeli walizoziandaa kuwaimbia Jumamosi.

Wachezaji wa Yanga wanaoonekana kupewa jukumu la kucheza kufa au kupona ili kukata ngebe za Simba Jumamosi ni kiungo Haruna Niyonzima, winga Simon Msuva na beki wa kati ambaye pia ni nahodha, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na mwenzake Kelvin Yondani.

Kwa bahati mbaya, nyota hao wamekuwa na wakati mgumu kila timu hizo zinapokutana wakidaiwa kutocheza katika kiwango chao hivyo kuwanyima raha mashabiki na viongozi wao.

Tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma, safari hii Msuva na Niyonzima wanakutana na Simba wakiwa katika kiwango cha hali ya juu kiasi cha kupewa nafasi kubwa ya kuwaangamiza Wekundu wa Msimbazi hao.

Lakini ifahamike kuwa nyota hao pamoja na wenzao, wanakutana na Simba Jumamosi huku wakifahamu jinsi mashabiki, wanachama na viongozi wao wanavyochekwa na watani wao hao wa jadi hivyo ni wazi kuwa watalazimika kupambana kadiri ya uwezo wao waweze kuwafuta machozi siku hiyo.

Katika hatua nyingine, wachezaji wa Yanga wametamba kucheza kadiri ya uwezo wao ili kuichapa Simba na hivyo kuwaziba midomo wapinzani wao.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Cannavaro aliliambia BINGWA mwishoni mwa wiki iliyopita akisema: “Mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi, waje kwa wingi uwanjani, japo mechi ni ngumu, lakini tumejipanga sawa sawa na kila mmoja wetu ana hasira na Simba, hasa kutokana na dharau zao dhidi yetu na viongozi wetu.”

Simba kwa sasa ndiyo inayoongoza ligi hiyo kwa kuwa na pointi 51 dhidi ya 49 za Yanga waliopo nafasi ya pili, lakini mabingwa watetezi hao wakiwa na mechi moja mkononi baada ya kushuka dimbani mara 21.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -