Tuesday, November 24, 2020

PAN AFRICAN NA HADITHI YA MWASHI ANAYELALA CHINI YA MTI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU

INAWEZEKANA isiwe na umaarufu sana kwenye kizazi hiki cha sasa, lakini Pan African ni moja kati ya klabu kongwe za soka nchini iliyoanzishwa mwaka 1975 baada ya kutokea mpasuko katika klabu ya Yanga uliosababisha baadhi ya viongozi wajitoe kwenda kuanzisha timu hiyo.

Licha ya ukongwe, umaarufu na mafanikio ya klabu hii katika miaka ya nyuma, leo Pan African imepotea kabisa na kubaki jina tu kitu ambacho kimezua maswali mengi ya nini kiliikuta klabu hiyo hadi kufikia hatua hii.

Kutokana na hali hiyo, BINGWA liliamua kuingia chimbo na kujaribu kutafuta ni wapi ilipo klabu hiyo na nini kinafanyika kuirudisha tena kileleni baada ya kupotea kwenye ramani ya soka la Tanzania.

Kuzaliwa kwa Pan African

Pan African ilizaliwa baada ya kuibuka kwa mgogoro ndani ya klabu ya Yanga, ambapo baadhi ya wachezaji walituhumiwa kuihujumu timu hiyo baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Enugu Rangers katika pambano la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga iliingia moja kwa moja raundi ya pili ya michuano hiyo baada ya kukosa mpinzani kwenye raundi ya kwanza. Katika hatua hiyo ilipangwa kukutana na Enugu Rangers ya Nigeria, ambapo katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Nigeria, timu hizo zilitoka suluhu lakini zilipocheza Dar es Salaam zikafungana 1-1. Yanga ikatolewa kwa sheria ya bao la ugenini.

Wachezaji waliodaiwa kuhujumu timu hiyo walifukuzwa lakini waliobaki nao wakaamua kutimka ikiwa ni ishara ya kutounga mkono wenzao kuondolewa kwenye kikosi hicho, kwa sababu timu ilitolewa kutokana na kuzidiwa kisoka na hapakuwa na kitu chochote nyuma ya pazia na hapo ndipo ukawa mwanzo wa kuzaliwa kwa Pan African.

Baada ya kuanzishwa Pan Africans iliibuka kuwa tishio nchini na mara kwa mara ilifanikiwa kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Afrika, ikicheza soka la uhakika mwaka 1979 timu hiyo ilikutana na AS Vita Club ya Zaire (sasa DRC) katika mashindano ya Kombe la Washindi sasa Kombe la Shirikisho Afrika. Hata hivyo, ilitolewa katika raundi ya pili kwa sheria ya bao la ugenini. Ilishinda nyumbani 2-1 na ziliporudiana mjini Kinshasa ikafungwa bao 1-0.

Katika raundi ya kwanza Pan African ilifanikiwa kuitoa Omedla ya Ethiopia kwa mikwaju ya penati 5-4, baada ya matokeo ya jumla kuwa sare ya bao 1-1. Pan ilifungwa nyumbani 1-0, ikashinda ugenini 1-0. Ikiwa katika kiwango cha hali ya juu, timu hiyo ilifanikiwa kushiriki mashindano hayo mwaka 1980 na ilikutana na Shooting Stars ya Nigeria.

Pan African ilitolewa tena katika raundi ya pili ya Kombe la Washindi kwa jumla ya mabao 2-1. Ilifungwa 1-0 nyumbani, na kulazimisha sare ya 1-1 ugenini. Katika raundi ya kwanza Pan iliitoa AC Sotema ya Madagascar kwa jumla ya mabao 5-4.

Mwaka 1982 Pan Africa ilishiriki tena Kombe la Washindi Afrika na safari hiyo ilitolewa kwa penalti 5-3 na Power Dynamos ya Zambia katika raundi ya pili baada ya kila timu kushinda bao 1-0 nyumbani kwao. Katika raundi ya kwanza Pan African iliishinda Mukura Victory Sports ya Rwanda kwa jumla ya mabao 8-0.

Ikiwa katika kiwango cha hali ya juu, timu hiyo ililitawala soka la Tanzania ambapo mwaka 1983, Pan African ilishiriki mashindano ya Klabu Bingwa Afrika sasa Ligi ya Mabingwa na kutolewa na Nkana Red Devils ya Zambia kwa mikwaju ya penalti 4-2 katika raundi ya pili baada ya mechi zote mbili kushindwa kuwa na magoli. Katika raundi ya kwanza Pan African iliitoa Wagad Mogadishu ya Somalia kwa jumla ya mabao 2-1.

Miongoni wa wachezaji waliokuwa wanawika na timu hiyo ni aliyewahi kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, ambaye aliiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Bara mwaka 1982, Juma Pondamali ambaye kwa sasa ni kocha wa makipa wa Yanga na straika Peter Tino.

Timu hii ambayo imewahi kuchezewa na mastaa kibao wa soka la Tanzania, mara ya mwisho kuishiriki Ligi Kuu ilikuwa mwaka 2007, lakini mvutano wa viongozi wake uliosababisha kupelekana mahakamani na kuvuruga taswira ya timu hiyo na kuporomoka hadi Ligi Daraja la Pili ngazi ya mkoa.

Mikakati ya kuirejesha

Hivi karibuni klabu hiyo ilifanya uchaguzi baada ya kuutimua uongozi uliosababisha timu hiyo kushuka daraja na kushindwa kuipandisha Ligi Kuu Tanzania Bara. Baadhi ya viongozi waliochaguliwa ni Salim Zagar (Mwenyekiti), Shabani Mtambo (Makamu Mwenyekiti), Peter Mushi (Katibu Mkuu).

“Tumelazimika kuunda kamati za kudumu ambazo tunaamini zitasaidia kuirejesha Pan African katika ubora wake. Wasimamizi wa kamati hizo wote wana uzoefu wa kuongoza soka na pia ni wanachama wa klabu hii hivyo Watanzania wasubiri kuiona Pan African mpya,” alisema Mushi.

Tenga ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji, Muhidin Ahmad Ndolanga kachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Nidhamu ya Klabu na wachezaji, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Fedha na Mipango na hawa wanaelezwa kuwa ni wadau wa soka la Tanzania.

Ile hadithi ya mwashi anayelala chini ya mti ndiyo iko katika klabu ya Pan African, kwa sababu licha ya timu hii kumiliki jengo lenye vyumba 13 katika Mtaa wa Swahili, Kariakoo jijini Dar es Salaam, timu hiyo haina ofisi ya kufanya shughuli zake kutokana na kupangisha vyumba vyote hivyo kwa wafanyabiashara.

“Ni jambo la aibu klabu kubwa kama hii kukosa ofisi, tumechaguliwa hivi karibuni ukweli ni kwamba shughuli zetu tunazifanya nje na ofisi. Uongozi tulioutoa madarakani umekodisha vyumba vyote kuacha kimoja ambacho tunaambiwa ofisi lakini kwa bahati mbaya hatujakabidhiwa hadi sasa na waliotangulia.

“Nia yetu ni kurudisha umoja ndani ya klabu ambapo tutapata muda mzuri wa kuiandaa vizuri timu yetu ili kuipandisha icheze ligi kuu msimu mmoja ujao,” alisema Mushi.

Kwa sasa klabu hiyo kongwe ina wanachama 75 pekee ambapo awali walikuwa wanazidi mara tatu ya idadi iliyopo na wanatarajia kufungua matawi mengine mikoani ikiwa ni moja ya kuongeza wanachama. Uongozi huo pia umepanga kuuza hisa kwa wanachama wa klabu hiyo kuongeza mapato ya timu hiyo ili isiwe tegemezi katika mifuko ya watu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -