Sunday, November 29, 2020

PASI ZA POGBA ZAWAFUNIKA VIUNGO LIGI KUU ENGLAND

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

ALIPOTUA Manchester United kwa ada ya usajili iliyovunja rekodi ya dunia, wengi walianza kumponda hasa alipoanza kwa mwendo wa kusuasua kikosini.

Lakini sasa, kiungo huyo ameonekana kuizoea Ligi Kuu England na tayari ameshaanza kutema cheche zake.

Hivi karibuni aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza Ligi Kuu England kufikisha zaidi ya pasi 1000 zilizowafikia walengwa.

Mpaka sasa, Pogba ana wastani wa kupiga pasi 42 katika kila mchezo, tena akifanya hivyo katika eneo la timu pinzani. Kwa takwimu hizo, kiungo huyo ana wastani wa asilimia 83 ya pasi sahihi.

Kwa takwimu hizo, takwimu za Pogba zinawapiku mastaa waliokuwa wakitamba kabla ya ujio wake Ligi Kuu England ambao ni Mesut Ozil, Eden Hazard na David Silva.

Akiwa na pasi 1029, Pogba anamzidi Jordan Henderson wa ambaye ndiye anayemfuata kwa pasi zake 987.

Mesut Ozil mwenye pasi 957 anashika nafasi ya tatu nyuma ya mastaa wenzake hao huku David Silva akiwa wa nne kwa pasi zake 930.

Huenda hilo limemjibu mkongwe wa Liverpool na mchambuzi wa soka katika kituo cha televisheni cha Sky Sport, Jamie Carragher, ambaye alisema Zlatan Ibrahimovic ndiye anayepaswa kushukuriwa kwa mafanikio ya Man United na si Pogba.

Pogba alirejea Old Trafford wakati wa majira ya kiangazi na ada yake ya rekodi ya dunia ilikuwa pauni milioni 89.

Hiyo ilikuwa ni miaka minne baada ya nyota huyo kuondoka bure Old Trafford na kujiunga na Juventus.

Mbali na rekodi hiyo ya pasi 1029 zilizowafikia walengwa msimu huu, Mfaransa huyo ameshapachika mabao  saba huku pasi zake za mwisho zikizaa mengine matatu.

Hata hivyo, wakosoaji wake wamedai kuwa staa huyo amekuwa akishindwa kung’aa katika michezo mikubwa hasa ile inayoikutanisha Man United dhidi ya timu zilizopo ‘top six’.

Moja ya michezo hiyo ni ule wa mwanzoni mwa msimu dhidi ya Manchester City na ule waliokutana na kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Chelsea.

Pia, kwa thamani yake na uwezo anaouonesha uwanjani, wakosoaji wanaamini kuwa ‘asisti’ tatu ni chache mno kwa mchezaji wa aina yake.

Kwa sasa Pogba ameonekana kutibu ugonjwa uliokuwa ukikisumbua kikosi cha kocha Louis van Gaal.

Wakati wa Van Gaal, Man United ilikuwa na tatizo kubwa katika pasi za kusogea katika eneo la hatari la timu pinzani, kitu ambacho sasa Pogba anakifanya kwa ufanisi mkubwa.

Kwa upande mwingine, ushirikiano mzuri kati ya Pogba na Ibrahimovic aliyetua bure Old Trafford, umekuwa na faida kubwa kwa safu ya ushambuliaji ya Man United.

Asisti zote tatu za Pogba zilizaa mabao ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Paris Saint-Germain ambaye alitua Ufaransa akitokea AC Milan.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -