Thursday, December 3, 2020

Pato: Pluijm hakunipa  nafasi Yanga

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA HUSSEIN OMAR

BEKI wa kati wa Yanga, Pato Ngonyani, amesema kama kocha mkuu wa kikosi hicho, Mholanzi Hans van der Pluijm, angempa nafasi ya kucheza mara kwa mara sasa hivi angekuwa kwenye levo nyingine.

Beki huyo alionyesha uwezo mkubwa katika mpambano wa watani wa jadi Simba msimu uliopita akicheza kama kiungo, mchezo ambao ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa Pato kucheza timu hizo mahasimu zilipokutana ambapo uwezo aliuonyesha uliwakosha mashabiki na sasa anadai kuwa kama angeendelea kuaminiwa na kupewa nafasi angekuwa mhimili mkubwa kwenye kikosi hicho.

Akizungumza na BINGWA, Pato alisema kama kocha wake akimpa nafasi kwenye mchezo wowote ataonyesha uwezo mkubwa kwani licha ya kwamba kuna idadi kubwa ya wachezaji katika kikosi chao hicho anaamini yeye ni mpambanaji.

“Mimi naamini kwamba ninacho kiwango kizuri na kama kocha akinipa nafasi katika mchezo wowote nitacheza kwa juhudi zangu zote ili kuwaaminisha hiki ambacho ninakisema,” alisema Pato.

Pato ni moja ya mabeki ambao wanatarajiwa kuziba nafasi za akina Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambao umri unawatupa mkono na muda wowote wanaweza kutundika daluga.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -