Sunday, January 17, 2021

Paul Pogba alikuwa katika ubora wake

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

Manchester, England

SOKA aliloonyesha Paul Pogba mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Leicester City, lilikuwa la kiwango cha juu tangu avae tena uzi wa Manchester United, alisema mchambuzi Gary Neville.

Lakini mchambuzi mwingine, Graeme Souness, atafurahi sana kumuona nyota huyo wa Ufaransa akichezeshwa nafasi ya mbele zaidi.

Pogba alipewa tuzo ya nyota wa mchezo wakati United wakiichapa Leicester mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Old Trafford, akifunga bao lake la kwanza tangu avunje rekodi ya usajili ya pauni milioni 89 akitokea Juventus majira ya kiangazi.

Wachambuzi hao wakizungumza kwenye televisheni ya Sky Sports baada ya mechi, Neville alisema Pogba alihusika katika mchezo wote, hasa kwa kazi yake nzuri ya kukaba, amezinduka baada ya kushindwa kuonyesha kiwango kizuri katika mechi zilizopita.

Neville alisema: “Pogba ndiye alikuwa kila kitu katika kipindi cha kwanza. Tunaangalia kutokuwepo kwa Wayne Rooney, lakini mchezaji mwenye thamani kubwa ni lazima utawale mchezo.

“Kipindi cha kwanza aling’ara uwanjani. Alionekana kutawala mchezo, kama kocha wake Jose Mourinho alivyomwelekeza na alipora mipira. Nafikiri alipigiwa simu wiki hii akaambiwa zinduka.

“Kila alichofanya alionyesha kiwango. Ni kiwango kizuri ambacho sijawahi kukiona kwake.

“Kama unataka kiungo wako mwenye thamani ya pauni milioni 89 afanye kitu, basi itakuwa ni kupiga pasi vizuri, kupanda mbele, kuwa tishio eneo la hatari, kuonyesha nguvu, kurudi nyuma kwa haraka na kukaba.”

Naye Souness anaamini atakuwa na mafanikio zaidi katika kuwasumbua mabeki na kuonekana sana kwenye eneo la hatari la wapinzani.

“Nafikiri Pogba anatakiwa awepo mbele mara kwa mara, awe anaingia ndani ya 18. “Anaonekana ana uwezo wa kukimbia,” alisema kiungo huyo wa zamani wa Scotland, Souness.

“Nitapenda kumuona akiwa ndani ya boksi zaidi, anakuwa tishio akiingia kwenye eneo hilo. Ana nguvu, anapambana, anaweza kupiga mipira ya kichwa, bila ya shaka anacheza vizuri. Ataonyesha mambo mengi zaidi na atakuwa ni mmoja wa wachezaji wenye mabao mengi.

‘‘Kama ningekuwa nacheza naye, ningekuwa nikifurahia kumuona akiwa mbele yangu muda wote, sitapenda kukimbia mbele kama yeye kwa kuwa anaweza kukukimbiza kutwa nzima.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -