Friday, October 23, 2020

PAYET JIANGALIE, HAWA WENZAKO WALIJUTIA MAAMUZI YAO BAADAYE

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

LONDON, England

SUALA la mchezaji kulazimisha kuondoka ndani ya klabu yake na kuanzisha visa huwa ni nadra kutokea na iwapo likitokea, ni lazima kuwe na mizozo inayosababisha timu husika kupoteza mwelekeo katika ligi.

Aidha, mzozo huo hauwezi kuwa mkubwa iwapo mchezaji ambaye analazimisha kuondoka hana nyota ya kupendwa ndani ya klabu.

Ni lazima awe staa anayetegemewa kutokana na nafasi yake uwanjani, kama alivyofanya kiungo wa klabu ya West Ham, Dimitri Payet, ambaye kocha wake Slaven Bilic, alithibitisha kuwa Mfaransa huyo anataka kuondoka huku mashabiki bado wakiwa wanampenda.

Lakini historia ya soka inaonesha mara tu baada ya mastaa hao kulazimisha kuondoka, maisha huwageukia na kuwa magumu huko waendako kama ilivyowahi kuwakuta mastaa hawa:

Nicolas Anelka

Anelka bado alisumbuliwa na hali ya ujana, hakujua nini anachokitaka maishani mwake akiwa kama kijana mdogo.

Ndani ya klabu ya Arsenal, Mfaransa huyu alianza kung’ara akiwa mdogo ambapo alitumika kama mshambuliaji wa kati huku akionesha uwezo mkubwa kwenye mfumo ambao baadaye ulikuja kumuibua Thierry Henry.

Henry alikuja kung’ara mno baada ya Anelka kutimkia Manchester City. Msimu ambao Arsenal inachukua ubingwa bila kufungwa na Henry akifunga mabao 30 ya ligi, Anelka ndio alitimiza mwaka wa tatu ndani ya klabu ya City ambayo ilimaliza nafasi ya 16 mwaka 2004.

Maisha ya Anelka kwenye soka yakawa ni ya kuhangaika huku na kule. Ni uhamisho wa kwenda Real Madrid mwaka 1999 akitokea Arsenal ndio ulimfurahisha, lakini hakupata nafasi kikosi cha kwanza kwa haraka na hata alipopata nafasi, alifunga mabao saba tu kabla ya Madrid kumuuza PSG miaka miwili baadaye. Tangu aikache Arsenal, Anelka amezichezea jumla ya timu 11.

Peter Odemwingie

Mnigeria huyu alitua England kwa mara ya kwanza akitokea Lokomotiv Moscow ya Urusi, ambapo West Brom ndio klabu iliyofanikiwa kuinasa saini yake mwaka 2010.

Mashabiki walimkubali mno ambapo kwa miaka mitatu aliyokipiga hapo alicheza jumla ya mechi 85 za michuano yote na kufunga mabao 30, ambapo alifunga mabao 12 ya Ligi Kuu England katika msimu wake wa kwanza.

Odemwingie aliibuka kuwa kipenzi cha mashabiki hasa kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao hata dhidi ya klabu kubwa kama Arsenal na Liverpool, mwaka mmoja baadaye Juventus walianza kummendea lakini klabu yake ilipiga chini ofa hiyo.

2013 aliomba kuondoka lakini West Brom ilimgomea, kabla ya kudaiwa kuwa alionekana nje ya ofisi za klabu ya QPR katika harakati zake za kutaka kujiunga na klabu hiyo, taarifa zilizowakera mabosi wake na kuamua kumuuza Cardiff City mwaka huo.

Hakudumu sana, akahamia Stoke City kabla ya kujikuta akiporomoka hadi Rotherham inayoshiriki ligi ya Championship England mwaka jana.

Darren Bent

Maisha ya Bent ndani ya klabu ya Sunderland yalikuwa mazuri mno. Akishirikiana na Asamoah Gyan kwenye safu ya ushambuliaji, kwa pamoja walizisumbua timu nyingi kutokana na uwezo wao wa kupachika mabao.

Matukio ya kufurahisha yanayokumbukwa ni sare ya bao 1-1 dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Newcastle mwaka 2011, Gyan akisawazisha bao dakika ya 90 na tatu za nyongeza.

Pia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mabingwa wa mwaka huo, Chelsea ulidhihirisha kuwa Bent hakuwa na shida ndani ya klabu hiyo.

Balaa lilianza pale Aston Villa waliokuwa kwenye janga la kushuka daraja walipoweka pauni milioni 18 mezani wakimtaka Bent mwaka huo huo, na mshambuliaji huyo alizitamani fedha akaanza kuisumbua klabu hadi walipoamua kunawa mikono na kumkubalia.

Aliichezea klabu hiyo kwa miaka minne, lakini mwaka 2015 alishuka nayo daraja kabla ya kuuzwa Derby County ambako anaichezea hadi sasa kwenye ligi ya Championship.

Emmanuel Adebayor

Mchezaji mwingine wa Arsenal ambaye alizibeba tabia za Anelka ni huyu, Emmanuel Adebayor.

Raia huyu wa Togo alikuwa na maisha mazuri pale Emirates, akishirikiana na Robin van Persie, waliunda safu kali ya ushambuliaji. Miaka mitatu ya kukipiga Arsenal (2006-2009) ikamalizika na akahamia Manchester City kwa uhamisho uliogharimu pauni milioni 25.

Ni uhamisho ambao haukuwafurahisha mashabiki wa Arsenal na akazidi kuwakera zaidi kwa kushangilia bao alilowafunga kwenye ushindi wa mabao 4-2 walioupata City dhidi ya Arsenal.

Hakudumu sana ndani ya klabu hiyo, kwani alitolewa kwa mkopo Real Madrid ambako alinyakua taji moja la Copa del Rey. Hata hivyo, kiwango chake hakikuwaridhisha miamba hao wa Hispania na wakamrudisha City.

Akatolewa tena kwa mkopo kwenda Tottenham ambako alikabiliwa na matatizo binafsi yaliyoshusha kiwango chake kwa asilimia kubwa. Kiujumla alihangaika sana na klabu yake ya mwisho kuichezea ni Crystal Palace lakini hakudumu akaachwa huru.

Scott Sinclair

Katika timu zote 14 alizowahi kuzichezea, Sinclair alifanya vizuri mno ndani ya klabu ya Swansea tu, ambako aliichezea jumla ya mechi 85 na kufunga mabao 28.

Winga huyo alitua Swansea mwaka 2010 baada ya kuzunguka kwa mkopo timu takribani tisa ndani ya miaka sita, alionekana kama amefika nyumbani.

Hata hivyo, miaka miwili ya kucheza soka safi ndani ya klabu hiyo hadi kupachikwa jina la ‘Swanselona’ ilionekana kutomtosha Sinclair, akaiambia klabu yake bila kusita kwamba anataka kuondoka.

Akaenda zake Manchester City mwaka 2012 ambako alicheza mechi 13 tu za ligi kuu! Ni kitu ambacho hakukitarajia kabisa, kwani mawazo yake yote alijua angepata nafasi ya kutosha ya kucheza hasa kutokana na kwamba alisajiliwa na mabingwa watetezi wa ligi.

Alipokumbuka anaenda kwenye timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, hamu ikamjaa lakini kumbe alienda kwenye shimo lililoua kiwango chake na akaishia kukaa benchi na wachovu Jack Rodwell na Mario Balotelli kabla ya kupelekwa Aston Villa ambayo alishuka nayo daraja, lakini kwa sasa angalau anafurahia maisha ndani ya klabu ya Celtic ya Scotland.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -