Wednesday, November 25, 2020

PENALTI SIMBA ZAVUNJA UNDUGU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY, ZANZIBAR

MATOKEO ya mikwaju ya penalti yaliyoipa ushindi wa mabao 4-2 Simba dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga, huenda yakawa yamejenga uhasama mkubwa miongoni mwa wachezaji wa timu hizo mbili, baada ya kushindwa kupeana mikono baada ya pambano hilo.

Kitendo hicho ambacho ni maarufu sana Zanzibar kwa sasa ambacho kinaitwa ‘kuvunja undugu’, kilitokea baada ya penalti ya mwisho ya Simba iliyopigwa na Javier Bokungu, kutinga wavuni na kuibua shangwe kwa upande wa Simba hali ambayo iliwanyong’onyeza Yanga ambao waliamua kutoka uwanjani kwa kasi.

Licha ya wachezaji wa Simba kushangilia na kutaka kupeana mikono na wachezaji wa Yanga, lakini hilo halikufanikiwa kwani benchi la ufundi la Yanga liliwatoa wachezaji wote kwa kasi ya ajabu na kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Kitendo cha kutopeana mikono ni maarufu sana visiwani humo baada ya wanasiasa wawili mahasimu ambao wote wanatoka Pemba, Maalim Seif Sharif Hamad kugoma kumpa mkono Rais wa Zainzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, mbele ya umati wa watu mwaka jana.

Kitendo cha wachezaji wa Yanga kukwepa kupeana mikono na wenzao wa Simba, nacho kiliibua sintofahamu  miongoni mwa mashabiki huku wengi wa mashabiki wa Simba wa Zanzibar wakisema wamevunja undugu.

Pamoja na kwamba hakuna ulazima sana wa kupeana mikono baada ya mpira kumalizika, lakini imezoeleka hivyo  kwa kuwa mchezo wa soka ni wa kiungwana hata kama utakuwa umefungwa.

Simba ilishinda kwa penalti baada ya kumalizika dakika 90 timu hizo zikiwa suluhu na kwa ushindi huo Simba wametinga katika fainali ya kombe hilo la Mapinduzi ambapo watakutana na Azam FC kesho Ijumaa.

Yanga walikosa penalti zao mbili za kipa Deo Munishi na beki wa kushoto, Hajji Mwinyi, huku kiungo Thaban Kamusoko na winga mahiri Simon Msuva, wakitumbukiza penalti zao zilizoipa Yanga mabao mawili kwenye mchezo huo wa nusu fainali.

Kwa upande wa Simba waliopata penalti zao ni nahodha, Jonas Mkude, kipa Daniel Agyei, Mzamiru Yassin na Javier Bokungu aliyefunga ya mwisho na ya ushindi ambapo Method Mwanjale yeye alikosa baada ya kipa wa Yanga kuipangua.

Katika hatua nyingine, mashabiki wa Simba wameacha shughuli zao na kwenda kuwapokea wachezaji wa Yanga katika Bandari ya Dar es Salaam, wakati walipowasili jana mchana kutoka Zanzibar.

Mashabiki hao waliovalia jezi za Simba, walikwenda kuwasubiri Yanga kwa lengo la kuwacheka na kuwazomea, hali iliyofanya wachezaji wa timu hiyo kushindwa kupanda basi lililoandaliwa na viongozi wao kwa kukwepa zomeazomea za mashabiki hao wa Msimbazi.

Kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya wachezaji wa Yanga kutoka bandarini kwa kuvizia huku wengine wakikataa kupanda basi lao na kutafuta usafiri binafsi ili kuepusha vurumai za mashabiki wa Simba waliotaka kuwazomea na wale wa Yanga ambao walikwenda kuipokea timu yao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -