Thursday, December 3, 2020

PEPE ANAONDOKA, VALLEJO ANAKUJA!

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

Na Markus Mpangala

NDANI ya dimba la Santiago Bernabeu kuna tabia moja ya kikorofi na ujeuri kutoka kwa mashabiki wetu. Real Madrid inapocheza na timu yoyote yenye mshambuliaji tishio basi kocha anatakiwa kumpanga Pepe Lima akiwa fiti na mchezo huo.

Mashabiki wakishamwona Pepe uwanjani wanaanza kumzomea mshambuliaji wa timu pinzani ili kumtoa mchezoni. Halafu wanamwambia “Pepe yupo leo, utakiona cha mtema kuni,”.

Kwao wanamwona Pepe kama mtibuaji. Mtu wa shughuli, mchapa viatu, na kiboko cha washambuliaji tishio. Wakija Luis Suarez, Lionel Messi, hata kijana wetu tuliyemuuza Pablo Leon au Aduriz na Griezmann wakikutana na Pepe maneno ya mashabiki ni yale yale, ‘piga huyoo! “Ua huyoo!

Pamoja na kupendwa kote huko na upole wake hali ya sasa Pepe kubaki Real Madrid ni finyu mno. Ni wazi sasa Pepe anaondoka klabuni. Kocha Zinedine Zidane amekubali sasa wakati wa Pepe kubaki kikosi cha kwanza umekwisha. Anamhitaji Raphael Varane sasa acheze na El Capitano Sergio Ramos.

Sio kitu rahisi hadi mashabiki kusema “Jesus Vallejo El Successor de Pepe” yaani Jesus Vallejo ni mrithi wa Pepe. Mwanzoni mwa msimu huu Real Madrid imefanya maamuzi magumu sana juu ya wachezaji wake.

Jesus Vallejo ni beki wa kati. Anacheza namna 4 na 5, ikibidi kiungo mkabaji na beki wa kulia. Amekulia Castilla. Akapelekwa Eintracht Frankfurt kwenye Bundesliga kule Ujerumani kupata uzeofu.

Sasa basi, ifikapo Januari 5 mwakani Vallejo atatimiza miaka 20. Huu ndio umri wa kuonyesha zaidi makeke yake katika kandanda. Ndio umri wa kupevuka na kutimiza ndoto yake aliyonayo ya kuvaa jezi za Los Blancos.

Vallejo alisajili kule Real Zaragoza mwaka juzi kwa pauni milioni 6 tu. Anakimbia, anamsuli na mabavu, anapiga viatu vya akili, halafu ana mapafu ya mbwa, hachoki haraka.

Hana presha ya mechi, mtukutu fulani awapo uwanjani, anaweza kuchukua nafasi ya nyimbo za “Muue huyoo!  Ingekuwa soka la kizamani huyu bwana mdogo ni mhuni sana uwanjani.

Taarifa za klabu zinasema kuwa Zidane sasa anahitaji kumwendeleza na kumrekebisha Varane, kwahiyo anamhitaji Jesus Vallejo arudi nyumbani kupokezana namba na Varane.

Kwa sasa Zidane anamwona Vallejo ameiva. Anaweza kukabiliana na presha, anaweza kuchuana na staa yoyote kupata namba kikosi cha kwanza. Ana chembechembe za ubishi kama Mariano Diaz.

Jambo jingine ambalo liliiletea presha Real Madrid ni kikosi cha dhahabu za Castilla kilichoibuka na wakali kibao.  Vallejo ni zao halisi ya Castilla kama walivyo wenzake akina Mariano Diaz, Diego Llorente (huyu amepelekwa Malaga na wakati wowote anaweza kurudishwa kusaidiana na Vallejo), Borja Mayoral, Martin Odegaard (amepelekwa uholanzi), Marcos Llorente (yuko kwa mkopo Alaves), Enzo Zidane, na Alvaro Tejero.

Wote hawa ni vijana waliopelekwa kwa mikopo kwenye klabu mbalimbali isipokuwa Enzo na Tejero. Huu ni ujumbe kwa wapinzani wetu kuwa Real Madrid imejaa vipaji na sasa inajivunia zaidi mapishi yake kuliko Galactico.

Kwa hali ninayoona itakuwa rahisi zaidi kwa Vallejo kumudu nafasi ya Varane kwakuwa Mfaransa huyo huwa ana tatizo la majeraha ya mara kwa mara.

Mchezaji mwingine mwenye uhakika wa kurudishwa haraka ni Marcos Llorente. Huyu ni kiungo mkabaji ambaye amejizolea umaarufu katika klabu ya Alaves. Alipelekwa kwa mkopo katika klabu huyo ili kukuza uwezo wake. Na sasa yuko tayari kusaidiana na Carlos Casemiro.

Kama unakumbuka vizuri uchezaji wa Xabi Alonso basi unatakiwa kwenda YouTube kumtazama Marcos Llorente yukoje. Tofauti ya Llorente na Vallejo ni moja; Vallejo ana usongo sana, mbishi na anacheza soka la shoka. Muda wote ni mtu wa kazi.

Lakini Marcos Llorente anapenda madoido, udambwidambwi na mikogo fulani awapo dimbani. Sifa yake kubwa ni macho makali katika kupanga mashambulizi. Ana zile pasi ndefu za Alonso, anapika mabao, ana kasi na mguu wake wa kushoto umejaa madini matupu. Akimpigia ndefu walau mbili tu kwa Alvaro Morata, unategemea nini? Subirini mambo!

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -