Thursday, December 3, 2020

‘Pepo’ ya Pogba katikati ya ubongo wa Herrera na Mata

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

HATIMAYE tumeiona sura halisi ya Jose Mourinho kwenye EPL, tumegundua kinachoitafuna Leicester na kitakakachomwondoa London, Antonio Conte.

Tumeiona thamani ya Paul Pogba na tumejiridhisha juu ya ubora  wa Mesut Ozil. Tumejua pia anachokimaanisha Klopp msimu huu na wapi anatakiwa kukaa Wayne Rooney. Tuanze na Pogba.

Asikudanganye mtu tena ‘Pepo’ ya Paul Pogba pale Old Trafford iko katikati ya mafundi wawili wa Kihispania, Juan Mata na Ander Herrera.

Herrera na Mata ndio wameishikilia furaha na thamani ya Pogba mbele ya nyuso za walimwengu, ile nafasi aliyocheza dhidi ya Leicester ndio nafasi anayotakiwa awepo siku zote atakazokaa Old Trafford.

Mbele ya Herrera na nyuma ya Mata, hapa utampenda Pogba. Kwanini? Tulia nikusimulie.

Bila shaka unamfahamu, Xavi Hernandez, mmoja kati ya viungo bora kuwahi kutokea duniani, fundi wa mpira aliyeipa mafanikio makubwa Barcelona aliwahi kusema kila walipokuwa wakikabiliana na Athetic Bilbao walikuwa wakiandaa watu wawili wa kumdhibiti Herrera.

Unajua kwanini? Herrera ni miongoni mwa viungo wachache wenye uwezo wa kucheza kama ‘defensive midfielder’ na ‘holding midfielder’ kwa wakati mmoja.

Anaweza kukaba na kupokonya mpira, anaweza pia kupandisha timu na kutengeneza nafasi kwa watu wa mbele, faida ya mtu huyu akisimama nyuma ya Pogba ni ipi?

Pogba hana kasi na ni mara chache sana kumuona akigombea mpira na kushinda, madhara yake huonekana timu inapokuwa na mpira.

Ili awe huru anahitaji mtu mwenye uwezo wa kupokonya mpira na kuanza naye mashambulizi, mtu pekee wa kuifanya kazi ni Ander Herrera. Kwa Fellaini, Mourinho alikuwa akijidanganya tu!

Kazi inayofanywa na Herrera nyuma ya Pogba ina thamani sawa na ile inayofanywa na Juan Mata mbele ya Pogba. Kwanini?

Mata ni mbunifu, mtulivu na mwenye jicho la mpira. Anahitaji utulivu wa sekunde tano tu, atengeneze nafasi au afunge.

Uwezo wake unampunguzia majukumu mengi Pogba, ni yeye atakayemfanya awe huru zaidi kufanya kile alichobarikiwa miguuni mwake, si uliona alivyokuwa akifurahi na mpira kwenye ile mechi dhidi ya Leicester?

Wale ndio watu wawili wanaoweza kuifanya Man United ing’ae kwa kumzunguka Pogba na Mata na Herrera ndio wenye funguo za furaha ya Jose Mourinho pale Old Trafford.

Ndio, ‘Pepo’ ya Jose Mourinho pale Old Trafford iko mikononi mwa Herrera na Mata, hana ujanja tena zaidi ya kuamua kumtumikia kafiri ili hadhi yake ipande.

Mata anatakiwa arudi kwenye kikosi cha kwanza na Wayne Rooney apumzike benchi. Kwa mfumo wa 4-2-3-1 anaoupenda Mourinho, Zlatan Ibrahimovic ndiye anayestahili kuwa straika mmoja wa mbele.

Wayne Rooney wa sasa si wa jana wala juzi, hana kasi na amepoteza shabaha yake mbele ya lango. Ubora wake umeshuka!

Huu ni wakati wa Mourinho kusoma vyema alama za nyakati, Marcos Rashford, anahitaji muda zaidi uwanjani kuliko kukaa benchi. Bado sijaipatia picha Man United itakavyokuwa pindi Mkhitaryan atakaporudi kwenye ubora wake.

Achana na United, uliiona vyema Leicester ilivyocheza pale Old Trafford? Kama uliifuatilia vyema na kugundua tofauti ya kiwango chao kwenye dakika 45 za kwanza na 45 za pili, utajiridhisha kuwa haikuwa bahati mbaya wao kufungwa na Arsenal na Liverpool.

Ulimtazama Riyad Mahrez? Mchezaji bora wa ligi msimu uliopita? Unafikiri ameisha? Hapana, pale Leicester amebakiza mwili tu, akili na moyo wake vyote viko Nou Camp, anasubiri wakati sahihi ufike tu.

Kile kilichowakuta Chelsea kwa Arsenal ni matokeo ya Arsene Wenger kurudia majibu ya mtihani aliowahi kuufanya dhidi ya Van Gaal kipindi kile alipoichapa Man United mabao 3 ndani ya dakika 20.

Zinapigwa pasi tatu, bao, pasi tatu tena, bao. Kwenye ngumi staili ile inaitwa ‘Counter punch’. Unapigwa za uso fasta fasta ukija kushtuka umeloa damu. Ni ngumu sana kucheza na ‘Wenger timamu’ anapoamua kufanya jambo lake.

Wenger amemkaribisha vyema Antonio Conte katika jiji la London na kumuonyesha kuwa pale ukiwa jeuri unakutana na majeruhi zaidi yake.

Funguo ya furaha ya Conte ipo kwa kuwapanga Oscar na Fabregas pamoja na kuacha ujinga wa kuwapanga Matic na Kante. Akiendelea kubishana na ukweli, atahukumiwa na ukweli hivyo hivyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -