Friday, November 27, 2020

PETER LIM; BILIONEA WA SINGAPORE ANAYEIMALIZA VALENCIA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MADRID, Hispania

BILIONEA Peter Lim ametumia fedha nyingi kujaribu kurejesha makali ya Valencia ambayo yameonekana kupotea katika miaka ya hivi karibuni.

Hata hivyo, bado ndoto ya mmiliki huyo wa Valencia mwenye utajiri unaotajwa kufikia Dola za Marekani bilioni 2.3, imeshindwa kutimia.

Alitumia kitita cha euro milioni 200 kuinunua klabu hiyo pamoja na kuifanyia marekebisho kadhaa.

Bilionea huyo hajaonekana uwanjani kuitazama timu hiyo tangu ilipoibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Eibar na hiyo ilikuwa mwanzoni mwa mwaka jana.

Nini alichokosea bosi huyo kiasi kwamba Valencia imeendelea kuteseka La Liga ikiwa inakamata nafasi ya 16 kwa sasa?

Kwanza, Lim ameshindwa kuweka nfumo mzuri wa michezo klabuni hapo. Mfano mzuri ni kitendo cha mkurugenzi wa michezo, Jesus Garcia Pitarch, kupenda kuuza wachezaji.

Kuuzwa kwa baadhi ya wachezaji tegemeo imekuwa sababu kubwa ya kikosi hicho kupoteza nguvu ya ushindani katika kuwania taji la La Liga.

Majira ya kiangazi yaliyopita, iliwapiga bei Andre Gomes, Shkodran Mustafi na Paco Alcacer na hapo iliingiza zaidi ya euro milioni 100.

Kabla ya hapo, tayari Valencia ilishayumba hasa baada ya kumuuza Otamendi ambaye alitua Ligi Kuu England na kujiunga na Manchester City.

Lakini pia, Valencia imeajiri na kutimua makocha watano na wakurugezi wa michezo wanne kwa kipindi kifupi kisichozidi miaka mitatu.

Miongoni mwa makocha waliokaa klabuni hapo kwa muda mfupi kabla ya kufungashiwa virago vyao ni Prandelli, Nuno Espirito Santo, Gary Neville na Pako Ayestaran.

Kosa kubwa lililowakera mashabiki ni kwamba, makocha hao hawakuwa na uzoefu na La Liga. Wengi waliamini kuwa Lim amewaajiri kiurafiki tu.

Mashabiki walifurahi kusikia wakala mwenye jina kubwa kwenye ulimwengu wa soka, Jorge Mendez, atakuwa bega kwa bega na klabu hiyo, wakiamini atawasaidia kunasa mastaa na kusimamia mchakato wa usajili.

Hata hivyo, Mendes ameshindwa kufikia matarajio ya wengi. Mwanzoni mwa mwaka huu, aliwaletea Eliaquim Mangala na Ezequiel Garay, lakini wameshindwa kuthibitisha thamani yao.

Lakini pia, Mendez ndiye aliyewasajili Aymen Abdennour na Ruben Vezo, ambao pia wamechemsha.

Hata wale wachache walioanza kung’ara waliishia kupigwa bei, akiwamo kiungo Andre Gomes, aliyejiunga na Barcelona.

Hivi karibuni, Rais wa Valencia, Layhoon Chan, alitangaza mpango wa timu hiyo kuachana na mtendaji mkuu, Anil Murthy.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, Layhoon yuko bize kwa sasa akisaka mrithi wake ambapo imeelezwa huenda akawa ni mmoja wa wachezaji wao wa zamani.

Lakini, mara nyingi wakongwe wa timu hiyo wamekuwa wakikataa kila wanapoitwa kushika wadhifa klabuni hapo, hivyo haijafahamika ni nani atakayekubali.

Valencia pia imeachana na aliyekuwa balozi wa timu hiyo kimataifa, Mario Kempes.

Mkataba wa mkongwe huyo ulifikia tamati Desemba 31, mwaka jana.

Imeripotiwa kuwa tayari uongozi wa juu wa Valencia umeshawasiliana naye na kumtaarifu kuwa hautampa mkataba mpya.

Taarifa hizo zilianza kusikika na kuenea haraka hivi karibuni hasa baada ya Valencia kupoteza matokeo katika mchezo waliovaana na Eibar.

Hiyo ilizua taharuki kubwa miongoni mwa mashabiki ambapo walimjia juu mmiliki Lim, wakishutumu utawala wake klabuni hapo.

Kempes amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Valencia hasa kutokana na tabia yake ya kumkosoa Lim na kupingana na sera mbovu za usajili.

Ujenzi wa uwanja wao wa Nou Mestalla umetajwa kuwa chanzo kingine cha kuimaliza Valencia ambapo inasemekana kuwa kiasi kikubwa cha fedha kilitumika katika zoezi hilo.

Mwanzoni mwa mwaka huu, mashabiki waliandamana wakishinikiza Lim kuiuza Valencia aliyoinunua mwaka 2014.

Kuonesha hasira zao, miezi kadhaa iliyopita, binti wa tajiri huyo raia wa Singapore, Kim Lim, alifanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki wa klabu hiyo.

Historia fupi ya Lim

Mshua huyo alizaliwa mwaka 1954 nchini Singapore. Ana watoto wawili aliowapata kutoka kwa mke wake wa zamani aitwaye Venus Teo. Lim ni miongoni mwa wafanyabiashara wasomi duniani. Alihitimu masomo yake katika Chuo Kikuu cha Western Australia.

Akiwa na umi wa miaka 20 pekee, alikuwa mfanyabiashara mzuri katika soko la hisa ambapo alikuwa akitengeneza dola 385 (842,784) kwa mwezi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -