Sunday, November 29, 2020

PETIT MAN AFUNGUKA YALIYOMKUTA LUPANGO, AMWELEZEA WEMA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA KYALAA SEHEYE

MENEJA wa msanii wa Bongo Fleva, Bill Nass na County Boy anayefahamika kama Ahmed Salum ‘Petit Man’,  ameongelea fedheha na hasara iliyomkuta alipokumbwa na kashfa ya kuhusishwa na dawa za kulevya na kujikuta akiswekwa lupango.

Katika mazungumzo na BINGWA juzi, Petit Man, alisema kitendo cha kukaa mahabusu kwa wiki moja kimempotezea fedha nyingi ambazo alikuwa amepanga kuingiza kwa wiki ile ili kuwafikisha hatua nyingine wasanii wake wanaomtegemea yeye kwa asilimia kubwa.

“Naumia sana nikizungumzia suala hili kwa sababu naona ni moja ya vitu ambavyo vilitaka kunitia umasikini, pesa (fedha) niliyoipoteza wiki ile ilikuwa ya kunitoa sehemu moja kwenda nyingine, ilikuwa nyingi na nilitarajia kufanya mengi sana,” alisema Petit Man.

Aliongeza kuwa mahabusu si sehemu nzuri kwani amejifunza mengi sana na amekumbana na watu tofauti ambao wengine ameweza kuwasaidia na wengine imeshindikana.

Akizungumzia kipigo alichodaiwa kupigwa, Petit Man, alisema kutangaziwa kupigwa ilikuwa kama fedheha kwake akikiri kwamba alipata misukosuko ya kawaida na si kipigo kama ilivyovumishwa.

“Nadhani Kamanda Sirro (Simon) ni askari mkubwa na msomi, sidhani kama anaweza kutoa adhabu isiyostahili na inayokiuka haki za binaadamu na mimi nilipata adhabu yangu kama mtuhumiwa na yote hiyo ilikuwa ni kupata ukweli na si mimi pekee, nadhani wengi walipata adhabu ili waseme, sasa huo uvumi mwingine mimi siutambui na huwa sipendi kuongelea  naona kama umeniletea fedheha kwenye jamii, kila mtu anatafsiri yake,” alisema Petit Man.

Aliongeza: “Mimi sina rekodi mbaya, nina imani hii adhabu kabla ya kuisha nitapewa ruhusa ya kufanya mambo yangu kwa uhuru, hakuna asiyenijua mimi ni mtu wa aina gani, napenda sana kushirikiana na watu wa aina zote na kumsaidia mtu pale ninapoweza.”

Akizungumzia sakata la aliyekuwa swahiba wake wa muda mrefu, Wema Sepetu, kuhama chama, alisema kila mtu ana mawazo yake na utashi wake hivyo kama ameamua kufanya hivyo, basi inabidi wao wawe wasikilizaji kwani Miss Tanzania 2016 huyo ana wazazi wake na kwamba hayo ni mapendekezo ya mtu.

Hata hivyo, aliweka wazi akisema: “Mimi na Wema bado ni familia moja japokuwa kila mtu ana kampuni yake, niliamua kutoka kwenda kwenye kampuni ili kujitafutia kipato na nitaendelea kushirikiana naye kwa kazi ambazo tulikuwa tukifanya.”

Pia alizungumzia ndoa yake na mkewe, Esma Kandili ‘Esma Platinumz’ ambaye ni dada wa msanii nguli wa Bongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’, akisema anaamini ndiye mwanamke aliyechaguliwa na Mungu na katu hatafikiria kwenda kwingine.

“Nina amini Esma ndiye mwanamke niliyechaguliwa na Mungu, tulijaribu kutengena ila ilishindikana na kujikuta kila mmoja akimhitaji mwenziye na sasa ndoa yetu imerudi, ifahamike ndiye aliyenipa heshima ya kuitwa baba baada ya kufanikiwa kupata mtoto aitwaye Taraj,” alisema Petiti Man.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -