Wednesday, October 28, 2020

Philippe Coutinho Fundi wa Anfield anayewatoa udenda Barca

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

 

MERSEYSIDE, England

PHILIPPE Coutinho alisajiliwa na Liverpool akitokea Inter Milan na uhamisho wake uligharimu  pauni milioni 8 tu.

Alipofika Inter mwaka 2018, Countinho hakuwa na namba kwenye kikosi hicho, kilichokuwa kikinolewa na mkufunzi Jose Mourinho.

Nyota ya Countinho ilianza kung’aa baada ya ujio wa Rafa Benitez, ambaye alionekana kumkubali Mbrazil huyo na kumpa nafasi ya kuingia uwanjani mara kwa mara.

“Alikuwa msaada mkubwa. Alinifanya nijiamini. Mazoezi yalikuwa mazuri na alikuwa akifanya kazi vizuri,” alisema Countinho, alipokuwa akimzungumzia Benitez.

Lakini, Benitez hakudumu Inter na hapo ndipo ukawa mwisho wa Coutinho kuendelea kutamba.

Alipelekwa kwa Espanyol kwa mkopo ambako alikutana na Mauricio Pochettino, ambaye anaifundisha Tottenham kwa sasa.

Baada ya kushindwa kufanya kile kilichowafanya Inter kumsajili kutoka Vasco Da Gama ya Brazil, Inter waliamua kumpiga bei na ndipo Liver walipomchukua rasmi.

Liver walifanikiwaa kuwapiku Southampton, ambao pia walikuwa wakimfukuzia nyota huyo wa kimataifa wa Brazil.

Countinho alitua Liver wakati wa utawala wa kocha Brendan Rodgers na hakuna aliyetarajia kuwa siku moja angekuwa dhahabu ya Merseyside.

Mwanzoni mambo yalikuwa hovyo kwa upande wa nyota huyo ambapo alikiri kushindwa kulizoea soka la England.

Hata hivyo, Rodgers alimvumilia na hata Countinho aliwahi kusema kuwa kocha huyo alimpa muda wa kutosha kuzoea mazingira ya England.

“Mwanzoni haikuwa rahisi kuzoea, (soka la England) linashangaza. Lakini si kuzoea tu. Inachukua muda kuendana na kasi. Kasi ndiyo kitu kikubwa. Huwezi kuzubaa hata dakika moja,” alidai Countinho.

Imeelezwa kuwa, aliyekuwa mpachikaji mabao hatari wa klabu hiyo, Luis Suarez, alikuwa msaada mkubwa wa Coutinho kutulia na kulizoea soka la England.

Licha ya ugumu aliopitia hapo mwanzoni, hivi sasa Countinho amekuwa lulu pale Anfield. Amekabidhiwa jezi namba 10, ambayo ina heshima kubwa klabuni hapo.

Jezi hiyo ilivaliwa na mkongwe John Barnes, ambaye aliiwezesha Liver kunyakua mataji mawili ya Ligi Kuu England.

Mbali na Barnes, iliwahi kuvaliwa pia na aliyekuwa kipenzi cha mashabiki wa Liver, Michael Owen, ambaye alijizolea umaarufu mkubwa Ligi Kuu England kutokana na umahiri wake wa kuwatesa walinda mlango wa timu pinzani.

Itakumbukwa kuwa, Owen aliwahi kutwaa tuzo ya Ballon d’Or akiwa na Liver, kabla ya kutimkia La Liga ambako alijiunga na matajiri wa Bernabeu, Real Madrid.

Huku mambo yakionekana kuwa mazuri kwa Liver, inayoongoza ligi, Countinho amekuwa msaada mkubwa kwenye mafanikio hayo.

Kutokana na makali hayo, tayari taarifa zimeibuka kuwa Barca wanataka kumnunua Coutinho.

Wakali hao wa Ligi Kuu nchini Hispania ‘La Liga’ wanataka kuhakikisha Countinho anaungana na MSN (Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar).

Ikumbukwe kuwa Barca ndio waliomnunua Suarez, ambaye alikuwa tegemeo kwenye safu ya ushambuliaji ya Liver.

Barca wamepanga kukiongezea makali kikosi chao wakati wa dirisha dogo la usajili la Januari na wanamuona Countinho kama mchezaji sahihi  kujiunga na kikosi chao.

Mashabiki wa Liver wana haki ya kubaki roho juu, hasa kutokana na uswahiba mkubwa  uliopo kati ya Countinho na Neymar, ambao wote wanakipiga katika kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil  ‘Selecao’.

Kuna shaka kubwa kuwa huenda  Barca wakamtumia vizuri staa wao, Neymar, kumshawishi Countinho kufungasha virago vyake England na kutua Hispania.

Mpaka sasa Coutinho ameshacheza mechi 11 za Ligi Kuu England na takwimu zimethibitisha kuwa ana msaada mkubwa kwenye kikosi cha Klopp.

Idadi hiyo ya mechi ni sawa na dakika 843 na amefunga mabao matano, huku pasi zake za mwisho asisti zikizaa mengine matano.

Lakini pia, nyota huyo ametengeneza nafasi 30 za mabao, huku akiwa na idadi hiyo ya mashuti.

Mashuti 17 ya Countinho yamelenga lango la timu pinzani, huku mengine 13 yakiwa fyongo. Amepiga pasi 562 na asilimia 84 ya pasi hizo zimewafikia walengwa.

“Nilichukua ubingwa wa fainali za kombe la dunia za vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 nikiwa na Brazil. Nilikuwa Inter wakati iliposhinda fainali za kombe la dunia kwa ngazi ya klabu na hata iliposhinda Kombe la Ulaya, lakini sikucheza. Nataka kushinda mataji nikiwa hapa,” alisema.

Katika mchezo dhidi ya Crystal Palace, ambao ulikuwa wa mwisho kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa, mkali huyo alitoa asisti mbili.

Lakini pia, wiki iliyopita, alipachika bao moja katika ushindi wa 3-0 walioupata Brazil mbele ya mahasimu wao, Argentina.

Kwa sasa amebakisha miaka mitatu na nusu kumaliza mkataba wake pale Liver na huenda mabosi wake hao wakatamani kubaki naye hata baada ya hapo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -