Wednesday, January 20, 2021

Pluijm ajisalimisha kwa Pato, Kaseke

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA HUSSEIN OMAR,

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, ameendelea kuyafanyia kazi matatizo kadhaa kwenye kikosi chake katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, jijini Dar es Salaam, huku safari hii akiwavaa kivingive, Pato Ngonyani na Deus Kaseke.

Yanga wanatarajia kushuka dimbani keshokutwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuwakabili Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa kutambua umuhimu wa mchezo huo, benchi la ufundi la timu hiyo likiongozwa na Pluijm, limeamua kuja kivingine na tayari limewapa mbinu mbalimbali wachezaji wake kuelekea katika mchezo huo.

Kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na jana, Pluijm na wasaidizi wake walionekana kutilia mkazo maeneo matatu muhimu.

Maeneo yanayoonekana kutiliwa mkazo na benchi hilo la ufundi ni safu ya kiungo, ulinzi na ile ya ushambuliaji.

Kwenye mazoezi hayo ya jana, BINGWA lilishuhudia Mholanzi huyo alionekana kumpanga mchezaji Ngonyani kucheza pacha na Kelvin Yondani katika eneo la walinzi wa kati.

Lakini pia, Pluijm alimjaribu Kaseke katika nafasi ya kiungo mkabaji.

Itakumbukwa kuwa kwa muda mrefu mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara wamekuwa na tatizo katika nafasi ya kiungo mkabaji, ambapo kocha huyo amekuwa akimtumia Mbuyu Twite katika nafasi hiyo.

Ni wazi Pluijm ameonekana kutaka kitu tofauti kuelekea katika mchezo huo wa kesho dhidi ya Mtibwa.

Winga huyo alionyesha umahiri wake mkubwa wa kupiga pasi ingawa alikosa sapoti ya wachezaji wengine wa timu hiyo, Thaban Kamusoko, Donald Ngoma, Beno Kakolanya na Malimi Busungu waliokosa mazoezi kutokana na kuwa na ruhusa maalumu.

Tangu kuondoka kwa mastaa; Method Mogela ‘Fundi’, Athumai Idd ‘Chuji’, Frank Domayo ‘Chumvi’, Juma Seif ‘Kijiko’, Wanajangwani hao wameshindwa kupata warithi sahihi wa wakali hao.

Kaseke alionyesha umahiri mkubwa katika mazoezi ya juzi na baadhi ya mashabiki wa Yanga waliofika Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, walikiri wazi kuwa wamepata mtu sahihi wa kuitendea haki nafasi hiyo.

Mbali na pasi za uhakika, Kaseke alionyesha umahiri wake wa kukaba na kupokonya mipira na huku pasi zake zikiwa kivutio kikubwa kwa waliofika uwanjani hapo.

Mara baada ya kumalizika mazoezi hayo, BINGWA lilipata nafasi ya kuzungumza na Kaseke ambapo winga huyo alisema anamudu kucheza vyema nafasi nyingi uwanjani ikiwemo ile ya kiungo mkabaji.

“Mimi mbona poa. Naweza kucheza popote pale nitakapopangwa, uwezo wa kufanya ninao,” alisema Kaseke.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -