Wednesday, November 25, 2020

PLUIJM ASAINI MIAKA MIWILI SINGIDA UNITED

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

RAMADHAN HASSAN, DODOMA NA SALMA MPELI, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa zamani wa Yanga, Hans Van Pluijim, leo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha Singida United iliyorejea Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na BINGWA jana mjini hapa, Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba, alisema wameamua kumpa mkataba huo kutokana na kuridhishwa na uwezo wake.

Mwigulu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, alisema kocha huyo atasaini mkataba huo ili kuipa mafanikio timu hiyo.

“Ni kweli Pluijim ametua Singida United ‘The Wind Power’, tutakuwa naye kwa miaka miwili na tutasaini naye mkataba kesho (leo) ili aisaidie timu yetu,” alisema.

Alisema kocha mzawa Fred Minziro, alisema kocha huyo atakuwa msaidizi wa Pluijim.

“Minziro hatuwezi kuachana naye ataendelea kuwa na sisi ila pia leo (jana) tumemtambulisha mchezaji wa kigeni, nitakutajia jina lake,” alisema Mwigulu.

Wakati huo huo uongozi wa timu umemsajili kiungo wa kimataifa wa Zimbambwe, Tafadzwa Kutunyi, kutoka timu ya Chicken Inn FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Zimbabwe kwa mkataba wa miaka miwili.

Katibu Mkuu wa Singida United, Abdulrahman Sima, alisema baada ya kuingia mkataba na mchezaji huyo, alirejea kwao Zimbabwe na kutakiwa kurudi nchini Juni mwaka huu kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Sima  alisema wamejipanga kuongeza wachezaji wengine wa kigeni, angalau wafike wachezaji watano au saba kulingana na sheria iliyopo.

Alisema wanaongeza beki wa kati, washambuliaji wawili na kiungo mkabaji ambaye amesajiliwa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -