Thursday, December 3, 2020

Pluijm ateka hisia za mashabiki Yanga

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA HUSSEIN OMAR

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, juzi aliziteka hisia za mashabiki wa timu hiyo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Pluijm ambaye alikuwepo uwanjani na kuishuhudia timu yake ya zamani ikiibamiza JKT Ruvu mabao 4-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, alionekana kuwa kivutio kwa mashabiki hao ambao licha ya kumwona akiiongoza timu yao walimfuata na kumpa mkono na wengine kupiga naye picha.

Mara baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo msanii wa Bongo Movie, Ummy Wenslaus ‘Dokii’, aliwaongoza wenzake kwenda katika gari alilopanda kocha huyo na kuanza kupiga naye picha huku wengine wakiimba nyimbo.

Kocha kocha kocha kocha kocha kocha huyu ndiye kocha wetu mwenye mafanikio, hakuna kama yeye, alisikika mmoja wa mashabiki na mwanachama wa timu hiyo, Mwanamtumu maarufu ‘Mama Yanga’ ambaye alimkumbatia Pluijm.

Akizungumza mbele ya mashabiki wenzake, Dokii aliliambia BINGWA kuwa Yanga wamepoteza jembe lililowapa mafanikio katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

“Huyu ni bonge la kocha, hakuna asiyejua Pluijm kaifanyia nini Yanga, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, mimi bado naamini mpaka Yanga kufika hapa ni juhudi zake,” alisema Dokii.

Pluijm amejiuzulu kuifundisha Yanga ikiwa ni baada ya uongozi wa timu hiyo kumleta kocha mpya wa timu hiyo, George Lwandamina kutoka Zesco ya Zambia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -