Tuesday, January 19, 2021

Pluijm atumbua jipu Yanga

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA HUSSEIN OMAR,

SIKU chache baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, kumrejesha Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ambaye alijiuzulu kuinoa timu hiyo mapema wiki iliyopita, Mholanzi huyo amefunguka na kuanika kilichomponza na kuufanya uongozi wa klabu yake hiyo kutafuta mbadala wake.

Pluijm alijiuzulu baada ya Yanga kumleta George Lwandamina, ili kubeba mikoba yake ambapo Mzambia huyo aliingia mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi hicho mara baada ya kumaliza mkataba wake na Zesco.

Kutokana na kujiuzulu kwa Pluijm, Nchemba aliamua kuingilia kati suala hilo na kufanya mazungumzo na kocha huyo takribani siku tatu ambapo sasa amekubali kuendelea kukinoa kikosi hicho cha Wanajangwani.

Awali, Mwigulu ambaye ni mpenzi na mwanachama wa Yanga, alianza mazungumzo na wachezaji wa timu hiyo na baadaye kuwashauri viongozi kumrudisha Pluijm.

Akizungumza na BINGWA jana, Pluijm alisema mazungumzo mazito kati yake na Mwigulu ndiyo yaliyomfanya abadilishe uamuzi wake wa kujiuzulu na kurejea kuendelea na kibarua chake cha kuifundisha timu hiyo ya Jangwani.

“Waziri Mwigulu ni mtu mkubwa sana, pia ni heshima kubwa mimi kama kocha kuzungumza na Waziri ni jambo la kujivunia sana kwangu, moja kati ya mambo aliyonisisitizia nihakikishe Yanga inatetea ubingwa wake msimu huu,” alisema Pluijm.

Katika hatua nyingine, Pluijm alisema nidhamu ndogo kwa wachezaji wa timu hiyo ni changamoto nyingine na kusababisha kufanya vibaya katika michuano ya kimataifa mwaka huu.

Pluijm alisema wachezaji wengi wa Tanzania wanapenda kubembelezwa, hawataki kupelekwa puta hali ambayo inawafanya wengi wao kupoteza viwango vyao na wengine kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

“Nidhamu ni changamoto nyingine inayowakumba wachezaji wengi wanashindwa kucheza katika viwango lakini pia muda wote wanapenda kubembelezwa kama watoto,” alisema Pluijm.

Mholanzi huyo tayari alishawaaga wachezaji wa timu hiyo na kukosekana kwenye mechi dhidi ya JKT Ruvu iliyosimamiwa na msaidizi wake, Juma Mwambusi, huku ikishinda 4-0.

Uongozi wa Yanga ulitaka kumwondoa Pluijm na wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa, Juma Pondamali na meneja Hafidh Saleh na kuwaleta Mzambia, Lwandamina atakayekuwa kocha mkuu, akisaidiwa na Charles Mkwasa, kocha wa makipa, Manyika Peter na meneja ni Sekilojo Chambua.

Pluijm, aliyezaliwa Januari 3, mwaka 1949, alikuwa anaifundisha Yanga katika awamu ya pili baada ya awali kufundisha kwa nusu msimu mwaka 2014, akimpokea Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts.

Pluijm alitaka kuondoka Jangwani baada ya kuiongoza Yanga katika jumla ya mechi 124, akishinda 77, sare 25 na kufungwa 22.

Katika mechi 19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare sita na kufungwa mbili, wakati katika mechi 106 za tangu mwaka jana, alishinda 66, sare 19 na kufungwa 20.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -