Monday, November 23, 2020

Pluijm awashika uchawi akina Ngoma

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY,

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amewashika uchawi wachezaji wake baada ya kusema walizembea kupata ushindi dhidi ya Simba, katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA juzi, Pluijm alisema uzembe wao ulitoa mwanya kwa Simba kutawala mpira na kusawazisha bao ambalo walitangulia kufunga.

Pluijm alisema kuwa washambuliaji  wake, akiwemo Donald Ngoma, Juma Mahadhi na  Amis Tambwe walishindwa kuonyesha soka safi, wakati Simba wakicheza  pungufu uwanjani baada ya kiungo wa Simba, Jonas Mkude kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mechi hiyo, Martin Saanya.

Alisema  washambuliaji  hao walishindwa kuzitumia vizuri nafasi walizozipata, lakini  uzembe wa mabeki wa kushindwa kulinda  bao ulisababisha Simba kusawazisha.

“Awali kikosi changu kilipambana na kupata bao la kuongoza dakika za mapema, lakini baadaye walionekana kuzidiwa na kutoa mwanya kwa Simba kushambulia mara kwa mara na kubadilisha matokeo.

Mara nyingi wachezaji wangu wamekuwa na kawaida ya kuridhika na matokeo pindi tu wanapoona wanaongoza na hivyo kutoa mwanya kwa wapinzani kutawala mchezo na hivyo ndivyo ilivyokuwa leo (juzi),” alisema Pluijm.

Alisema kikosi chake kilionekana kuzidiwa zaidi kipindi cha pili, hali iliyosababisha wapinzani wao kutumia nafasi hiyo vizuri na kuwazidi ujanja na kupata bao.

Kwa matokeo hayo, Yanga wamefikisha pointi 11 ikiwa  nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo, huku  Simba wakiwa kileleni kwa pointi 17.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -