Friday, October 30, 2020

Pluijm: Ilikuwa lazima Chirwa afunge bao

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SALMA MPELI,

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amesema alimwandaa vya kutosha kisaikolojia mshambuliaji wa timu hiyo, Obrey Chirwa, ili aweze kufunga bao katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Yanga ilishinda mabao 3-1 huku Chirwa akianza kufunga mengine yakiwekwa kimiani na Simon Msuva na Donald Ngoma.

Chirwa lilikuwa ni bao lake la kwanza kuifungia Yanga baada ya kusajiliwa katika dirisha dogo la Shirikisho la Soka Afrika wakati timu hiyo ilipotinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho na kushindwa kuonyesha makali yake.

Akizungumza na BINGWA juzi, Pluijm alisema aliamini kwamba Chirwa lazima angefunga, kwani mara kwa mara alikuwa anampa moyo na kumwambia alisajiliwa baada ya kumwona ni mshambuliaji mzuri.

Pluijm alisema aliamini kwamba Chirwa atakuja kufanya vizuri siku moja kama ambavyo juzi alianza kufunga katika mechi muhimu dhidi ya Mtibwa Sugar.

“Binafsi nilikuwa naumia sana na kujikuta nikikata tamaa, lakini juzi amefunga na alinifuata na kunishukuru.

“Nilikuwa nampa matumaini siku zote kuwa yeye ni straika mzuri, hivyo asife  moyo kwa kushindwa kufunga kwani ipo siku atawashangaza watu ambao walimkatia tamaa  na kutaka asicheze tena na hilo limejidhihirisha leo (juzi),” alisema Pluijm.

Alisema licha ya Chirwa kufunga bao hilo, lakini alionyesha soka safi tofauti na siku zote alizocheza.

Akizungumzia kuhusu baadhi ya wachezaji akiwemo Ngoma, Haruna, Mbuyu Twite kuanzia benchi, Pluijm alisema alifanya hivyo ili kusaidia kuongeza nguvu katika dakika za mwisho.

Pluijm alisema kwa sasa anautazama mchezo wao dhidi ya Azam utakaochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Uhuru, kwani anaamini utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu hiyo kupoteza michezo minne mfululizo.

“Siwezi kuizungumzia sana mechi hiyo, lakini naamini maandalizi ndio msingi wa matokeo mazuri, sisi tunajiandaa na wao pia na dakika 90 zitajibu hayo,” alisema.

Katika hatua nyingine, kocha huyo alimpongeza winga wa timu hiyo, Simon Msuva, kwa kufikisha idadi ya mabao 50 kuifungia timu yake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -