Wednesday, October 28, 2020

PLUIJM KUENDELEZA DOZI YAKE NDANDA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

 

NA FAUDHIA RAMADHANI


 

BAADA ya Azam FC kuichapa Mbeya City mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara, kocha wa timu hiyo, Hans van der Pluijm, amesema anajipanga ili ahakikishe anatoa dozi nyingine kwa Ndanda katika mchezo utakaochezwa Jumatatu ya wiki ijayo.

Akizungumza na BINGWA juzi baada ya kushinda dhidi ya Mbeya katika Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi, alisema haikuwa rahisi kupata matokeo hayo.

Pluijm alisema mchezo huo ulikuwa mgumu, hivyo wanatarajia kufanyia kazi mapungufu ili waweze kuibuka na ushindi katika mchezo utakaofuata.

“Nimefurahi kupata ushindi, mchezo ulikuwa mgumu, lakini vijana wangu walipambana na baadaye kupata pointi tatu muhimu,” alisema Pluijm.

Katika hatua nyingine, Kocha wa Mbeya City, Ramadhani Nsanzurwimo, amewatupia lawama waamuzi kutokana na kushindwa kuzingatia sheria 17 za soka.

Nsanzurwimo alisema waamuzi walionyesha upendeleo kwa wapinzani na kusababisha kupoteza mchezo huo.

“Waamuzi walichezesha mchezo upande mmoja, ile penalti aliyosababisha kipa wa Azam (Razack Abalora) alistahili  kuonyeshwa kadi nyekundu kwa sababu alikuwa mchezaji wa mwisho katika eneo la hatari, lakini alionyeshwa ya njano,” alisema Nsanzurwimo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -