Monday, January 18, 2021

PLUIJM RASMI AZAM 100%

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAINAB IDDY

AZAM wamepiga hesabu kali zitakazotoa jibu sahihi la kuiwezesha timu yao kufika mbali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika na kuamua kusuka mpango mahususi wa kuhakikisha wanamng’oa rasmi kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm.

Mpango wa Azam kumwajiri Pluijm ulikuwa wa muda mrefu baada ya Yanga kumleta kocha mpya, George Lwandamina, wakati Pluijm alipotangaza kuachia ngazi kabla ya kurejeshwa na kupandishwa cheo kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, cheo ambacho haonekani kukifurahia sana.

Habari zilizopatikana ndani ya klabu ya Azam zilieleza  kuwa walianza kumpigia chapuo Pluijm kabla ya kuwatimua makocha wao wiki iliyopita kutokana na kufanya vibaya mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Pamoja na Azam kufanya siri, lakini BINGWA limeambiwa kwamba, kuna uwezekano mkubwa Pluijm atakangazwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo na kuanza kazi rasmi baadaye mwezi huu.

Chanzo hicho kilisema Pluijm ameridhia kuifundisha Azam inayokabiliwa na michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika itakayoanza mwezi ujao, lakini kwa sasa hawezi kuanika kila kitu hadharani kutokana na ukweli kwamba bado Pluijm ni mwajiriwa wa Yanga.

“Kwa sasa suala la kocha mpya wa Azam linashughulikiwa na mmiliki mwenyewe wa klabu hiyo, Yusuph Bakhresa na hataki kuwatumia watu wa kati kama walivyofanya kwa makocha wengine, Bodi ya Azam imegundua mambo kadhaa ambayo hawataki kuyaweka wazi, lakini kuhusu suala la Pluijm ni kweli na wakikubaliana basi huenda akatangazwa rasmi,” kilisema chanzo chetu.

Mtoa habari wetu alisema uongozi wa klabu hiyo umevutiwa na uzoefu wa Pluijm alionao kwenye michuano ya kimataifa na umeona hauwezi kuingia kwenye michuano hiyo mwezi ujao wakiwa na kocha wa muda ndiyo maana wanafanya mpango wa haraka kumalizana na Pluijm.

Kwa upande wake Pluijm hakutaka kuzungumzia suala hilo kabisa kwa madai kwamba yeye ni mwajiriwa wa Yanga. “Nilidhani unaniuliza kuhusu Yanga, hili suala tuliache ila ninachoweza kusema ni kwamba mimi ni kocha na kazi yangu ninayoipenda ni kufundisha timu,” alisema kwa ufupi.

Habari zaidi zilieleza kwamba, Azam walitupa ndoana kwa kocha mwingine wa zamani wa Yanga, Ernie Brandts, lakini chaguo lao limekuwa kwa Pluijm kutokana na kuwa na wasifu mzuri kwenye soka la Afrika.

Wiki iliyopita Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba, alisema wako kwenye mchakato wa kumpata kocha mwenye rekodi nzuri katika klabu yake na michuano ya kimataifa ili aweze kuifundisha timu yao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -