Saturday, October 31, 2020

Pluijm: Tutavunja mwiko Moro J5

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

BAADA ya juzi kufanikiwa kuwalaza Simba mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amesema kikosi chake kipo kamili kuvunja mwiko wa kufungwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro. Yanga watashuka kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuwavaa Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajia kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na upinzani mkali uliopo baina ya timu hizo mbili zinapocheza katika uwanja huo. Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, wameondoka leo asubuhi jijini Dar es Salaam kwenda mjini Morogoro tayari kwa mechi yao dhidi ya ‘Wakata Miwa’ hao. Akizungumza na BINGWA jana, Pluijm alisema wamepania kuhakikisha safari hii wanavunja mwiko wa kukosa ushindi katika dimba la Jamhuri kwa takribani miaka minne mfululizo. Alisema wamejiandaa vya kutosha kuhakikisha wanaendeleza wimbi lao la ushindi katika mechi za Ligi Kuu Bara kama walivyofanya kwenye mechi zilizopita. Alisema vijana wake wapo tayari kwa pamabano hilo wameamua kuondoka asubuhi ya leo ili vijana wake waweze kupata muda mzuri wa kupumzika. “Morali ya wachezaji ipo juu sana, tumetoka kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba, tunakwenda Morogoro kutafuta pointi nyingine tatu muhimu zitakazotufanya tuzidi kupaa kileleni mwa ligi,” alisema Pluijm. Pluijm alisema anatambua Mtibwa Sugar wana kikosi kizuri ambacho kimekaa pamoja kwa muda mrefu, hivyo anategemea kupata ushindani wa hali ya juu. “Tumejiandaa kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo wa Jumatano, natambua utakua ni mgumu kwa sababu Mtibwa watakua nyumbani wakihitaji pointi tatu muhimu, lakini hata sisi tunakwenda Morogoro kuhakikisha tunapata pointi tatu pia,” alisisitiza Pluijm. Yanga ndio wanaongoza ligi wakiwa na jumla ya pointi 12 sawa na Azam, lakini mabingwa hao watetezi wa ligi hiyo wapo kileleni kutokana na wastani mzuri wa mabao.

Previous articleSIRI YA MAUAJI SIMBA
Next articleKerr alia na Tambwe
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -