Sunday, November 1, 2020

Pochettino atarudia kile alichomfanyia Guardiola pale Camp Nou?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

KAMA ulikuwa hujui, Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino, ataendelea kubaki kichwani mwa mwenzake wa Manchester City, Pep Guardiola.

Kesho, wawili hao watakutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, lakini hii si mara yao ya kwanza kuvaana.

Guardiola na Pochettino walianza kuonyeshana kazi wakati walipokuwa na klabu tofauti Ligi Kuu Hispania, La Liga.

Pochettino alianza kazi ya ukocha mwaka 2009 akiwa na Espanyol na kipindi hicho alikuwa kijana mdogo tu, miaka 36.

Ushindi wake wa kwanza akiwa kocha wa Espanyol aliupata katika mchezo dhidi ya Barca, iliyokuwa ikinolewa na Guardiola.

“Espanyol walikuwa mkiani mwa msimamo wa La Liga na Barcelona walikuwa kinara, na kabla ya mchezo kila mmoja aliona tungefungwa, hatukupewa nafasi kabisa. Ulikuwa ni ushindi wa kipekee na usioweza kusahaulika,” alisema Pochettino.

Mpaka wanakutana, Barca walikuwa kileleni kwa tofauti ya pointi 10, lakini hilo halikumzuia Pochettino kuchukua pointi baada ya kikosi chake kushinda mabao 2-1.

Awali, Espanyol hawakuwahi kushinda dhidi ya Barca kwa kipindi cha miaka 27.

Kabla ya kuvaana na Pochettino, Barca walikuwa wameshinda mabao 4-0, huku Almeria na Deportivo wakikumbana na kichapo cha mabao 5-0 kila moja.

Atletico Madrid walitoka Camp Nou wakiwa hoi baada ya kulambwa mabao 6-0.

Barca walikuwa wameshinda mataji mengi, yakiwemo ya La Liga, Copa del Rey, Ligi ya Mabingwa Ulaya, European Super Cup, Spanish Super Cup na Kombe la Dunia kwa ngazi ya klabu.

Kwa upande wao, Espanyol hawakuwa wameshinda hata mchezo mmoja wa ligi, licha ya kushuka dimbani mara 14.

Walipotua Camp Nou, walikuwa wametoka kuchapwa mabao 2-0 na Sevilla, tena wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Kipindi hicho, kikosi cha Barca kilikuwa kimesheheni mastaa kama Ronaldinho, Eto’o, Henry, Yaya Toure, Abidal, Puyol na Iniesta, wakiwa kwenye ubora wao.

Baada ya mchezo huo, Guardiola alionekana kuikubali aina ya uchezaji wa Espanyol ambapo alisema: “Kuna timu zinazokusubiri na kuna ambazo zinakutafuta, Espanyol wanakutafuta.”

Hata hivyo, haikuwa rahisi kwa Espanyol kuhimili vishindo, kwani mara kadhaa Thierry Henry, Xavi na Lionel Messi walikuwa tishio mbele ya safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Kutokana na aina ya uchezaji wa Espanyol, staa wa Barca, Seydou Keita, alijikuta akishindwa kuhimili presha na hatimaye akalimwa kadi nyekundu.

“Hata hivyo (kuifunga Barca) unahitaji kuwa na bahati pia,” alisema Pochettino baada ya mchezo huo.

Itakumbukwa kuwa kabla ya kuchukua kibarua cha kuinoa Espanyol, Pochettino alikuwa beki wa kikosi hicho.

Kitendo cha kukabidhiwa benchi la ufundi kilionekana kama kamari kwani kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 36.

Alipokuwa Espanyol, alihusishwa na mpango wa kuwasajili mastaa Hernan Crespo na Mario Balotelli, lakini mpango huo ulisitishwa.

Lakini pia, Pochettino alikuwa na msaada mkubwa kutoka kwa staa Ivan de la Pena.

Hata hivyo, mwaka 2010, Espanyol ya Pochettino ililala mabao 5-1 mbele ya Barca.

Hicho kilikuwa ni kipigo chao cha mwisho na baada ya hapo Pochettino alicharuka na kushinda mechi nane kati ya 10 na mwisho wa ligi timu hiyo ilikamata nafasi ya 10.

Mafanikio hayo ndiyo yaliyoivutia Tottenham na ndipo walipomwajiri Pochettino.

Ikiwa chini ya Koch huyo raia wa Argentina, Tottenham imeonekana kuimarika na msimu uliopita ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu, nyuma ya mahasimu wao Arsenal na mabingwa Leicester City.

Lakini, Pochettino anaingia kwenye mchezo huo akiwa na kumbukumbu nzuri ya mchezo wa mwisho uliozikutanisha Spurs na Man City.

Walipokutana katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England msimu uliopita, Man City, iliyokuwa chini ya Manuel Pellegrin, ilichomoza na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya wapinzani wao hao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -