MANCHESTER, England
KIUNGO Paul Pogba amewakimbiza wachezaji wenzake wa Ligi Kuu England kwa mauzo ya jezi.
Manchester United walimnunua kiungo huyo kwa pauni milioni 89 majira ya kiangazi na kumnasa nyota huyo wa Ufaransa na sasa fedha yao waliyoitumia imerudi kutokana na mauzo ya jezi ya mchezaji huyo.
Zlatan Ibrahimovic anashika nafasi ya pili, akifuatiwa na nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez na Mesut Ozil wakishika nafasi ya tatu na nne.
Kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho anashika nafasi ya tano, huku David De Gea na Marcus Rashford (Manchester United) wakiwemo kwenye orodha ya wachezaji 10, pamoja na Sadio Mane (Liverpool), Dimitri Payet (West Ham) na winga wa Chelsea, Eden Hazard.