Sunday, January 17, 2021

POGBA: KWA MATIC HUYO MBONA MTANIKOMA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

KWA Matic huyo mbona mtanikoma, hivi pengine ndivyo anavyosema kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Paul Pogba, baada ya kumsifia staa wao mpya, Nemanja Matic, akidai kuwa atamsaidia kung’ara zaidi msimu huu.

Staa huyo raia wa Serbia, amekuwa akifanya vizuri katika kikosi hicho cha Jose Mourinho, tangu alipojiunga nacho kwa ada ya pauni milioni 40 akitokea kwa mabingwa wa Ligi Kuu England, Chelsea.

Katika michezo hiyo, Matic na Pogba,  walicheza pamoja na kuonesha kiwango kizuri hususani katika  wakati wa mechi  iliyopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita ambayo waliondoka na ushindi wa mabao  4-0  dhidi ya timu za West Ham na  Swansea City.

Katika msimu wake wa kwanza, nyota huyo wa zamani wa Juventus hakuweza kuonesha thamani iliyomfanya asajiliwe kwa pauni milioni 89.3, lakini kwa sasa anasema kuwa anavyoamini wakati atakapokuwa akicheza sambamba na Matic, itamfanya acheze kwa uhakika zaidi.

“Mara zote nilikuwa nikicheza kwa kujihami zaidi na sasa ninachokiwaza pia ni kushambulia zaidi kutokana na kuwa Matic naye atakuwa akicheza kama mlinzi,” staa huyo aliuambia mtandao wa ESPN.

“Sasa tunaweza kubadilishana na katika michezo yote miwili nimekuwa nikishambulia na huku yeye akiwa nyuma yangu,” aliongeza Mfaransa huyo.

Alisema kwa kucheza hivyo itamsaidia kwenda mbele licha ya kuwa atakuwa akicheza katika nafasi ya kukaba na atakuwa akisogea ili kuwasaidia washambuliaji jambo ambalo litamfanya aweze kupata mabao mengi.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -