Sunday, November 29, 2020

POLISI WALIONDOKA UWANJANI BAADA YA YANGA KUFUNGWA BAO LA NNE NA SIMBA 1994

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HENRY PAUL

MIONGONI mwa matukio yaliyowahi kushangaza wapenzi wa soka nchini ni lile lililotokea katika mechi ya Simba dhidi ya Yanga, ambapo polisi wenye sare walitoka uwanjani baada ya Simba kuifunga Yanga bao la nne.

Tukio hilo lilitokea katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (sasa ligi kuu), uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam (sasa Uhuru), siku ya Jumamosi Julai 2, 1994.

Tukio lenyewe lilikuwa hivi, katika dakika ya 39 ya kipindi cha pili mara baada ya mshambuliaji wa Simba, Dua Said kufunga bao la nne, zaidi ya polisi 100 waliokuwa wamevalia sare walianza kujikusanya kwenye lango kuu la kaskazini mwa uwanja na kutoka nje na kuacha kazi ya ulinzi iliyowapeleka uwanjani hapo.

Mashabiki wa Simba wakiongozwa na kikundi chao cha ushangiliaji cha Kidedea, walikuwa wakishangilia kwa kuimba Lipuli, Lipuli, Lipuli… wakimaanisha timu ya Lipuli kutoka Iringa ambayo nayo ilichapwa na Simba idadi hiyo hiyo ya mabao manne wiki moja nyuma.

Mashabiki hao wa Msimbazi walifanya hivyo wakiifananisha Yanga na timu hiyo ya Iringa.

Kama vile wapenzi hao wa Simba walikuwa wakijua timu yao itaibuka na ushindi siku hiyo walikuwa wachangamfu tangu mchezo haujaanza huku wakiimba wakisema kuwa Yanga ni kipigo tu. Wengi wa mashabiki wa Simba walikuwa na matarumbeta.

Simba iliingia uwanjani ikitokea visiwa vyenye maradhi ya karafuu, Zanzibar ambako ilikuwa imeweka kambi yake ambapo Yanga yenyewe ilitokea Bagamoyo maeneo ambayo timu zote zimekuwa na kawaida ya kuweka kambi kabla ya kukutana.

Katika mchezo huo Simba ilipata bao lake la kwanza katika dakika ya 16 lililofungwa na beki George Masatu kwa mpira wa adhabu. Masatu ambaye alikuwa hana kawaida ya kupiga mipira ya adhabu alikwenda mbele na kupiga mpira kiufundi na mpira ukampita juu kipa Stephen Nemes na kutinga wavuni. Ilikuwa nje kidogo ya eneo la hatari.

Katika dakika ya 33 Yanga walisawazisha bao hilo kwa mpira wa adhabu uliopigwa na Costantino Kimanda baada ya mchezaji mmoja wa Simba kufanya madhambi.

Furaha ya mashambiki wa Yanga ya kusawazisha bao haikudumu, kwani dakika mbili baadaye kona iliyochongwa na Masatu ilitua kwenye kichwa cha Athumani China na mpira kujaa wavuni.

Mpaka dakika 45 za kipidi cha kwanza zinamalizika, Simba walikwenda mapumzikio wakiwa mbele kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kutawala karibu sehemu zote za uwanja. Ilipata bao la tatu lililofungwa na mashambuliaji Madaraka Seleiman. Madaraka alifunga bao hilo baada ya kutanguliziwa pasi na George Lucas na kufukuzana na beki Salum Kabunda na kupiga kiki kali ya chini chini lililokwenda kutinga wavuni huku Stephen Nemes akijitahidi kudaka bila ya mafanikio.

Simba lifunga kitabu cha mabao katika dakika ya 39 ya kipindi cha pili lililofungwa na Dua Said aliyepokea kasi kutoka kwa Madaraka Seieleman. Hivyo hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika Simba walitoka uwanjani vifua mbele kwa kuwafunga Yanga mabao 4-1.

Simba: Mohamed Mwameja, Godwin Aswile, Deo mkuki, Mustapha Hoza, George Masatu, Iddi Seleiman, Athumani China, Hussen Marsha/George Lucas, Madaraka Seleiman, Edward Chumila (marehemu) na Dua Said.

Yanga: Stephen Nemes, Seleiman Mkati, Kenneth Mkapa/Willy Martin, Salum Kabunda, Constantino Kimanda, Nico Bambaga (marehemu), Mohamed Husseim ‘Mmachinga’/Ally Yusuf ‘Tigana’, Sekilojo Chambua,Said Mwamba ‘Kizota’ (marehemu), James Tungaraza ‘Bolizozo’ na Edibily Lunyamila.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -