Friday, October 30, 2020

PONDAMALI AWACHANA LAIVU WABAYA WAKE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR

KOCHA wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali, amevunja ukimya na kusema kuwa ataendelea kuwapo ndani ya kikosi hicho licha ya ‘figisu figisu’ za kutaka kumwondoa zinazofanywa na baadhi ya makomandoo wa timu hiyo.

Akizungumza na BINGWA jana, Pondamali alisema anazo taarifa zote juu ya mizengwe anayopigwa na baadhi ya makomandoo wa Yanga pamoja na wale wa Simba ili kumchanganya akili yake.

“Mimi kila kitu naelewa, nikwambie tu, sitaweza kumtukana mtu wala kumjibu najua kuna watu wanaojiita makomandoo, hao wenyewe wanajifanya wanajua kila kitu ndiyo maana wameacha shughuli zao ni kunitafutia mabaya.

“Mimi nafanya kazi ya taaluma ambayo nimeisomea, maisha ya kuomba omba siyawezi hata kidogo na siku zote watu wenye majungu hawafanikiwi,” alisema Pondamali.

Kuhusu makomandoo wa Simba, Pondamali alisema wanamfanyia ili awafanyie vurugu afungiwe kitu ambacho amesema hakiwezekani.

“Hawa makomandoo wa Simba na wenyewe wametia mkono katika suala langu zima la kutaka mimi niondolewe, lakini nawaambia kuwa sitamjibu wala kumtukana mtu,” alisema.

Alisema katika miaka yake mitatu aliyokaa na timu hiyo, anajivunia mafanikio mbalimbali aliyowapa Yanga na kusisitiza bado ataendelea kujituma katika kuhakikisha anawainua makipa wa timu hiyo ndiyo maana hata kocha mkuu George Lwandamina ameridhika kufanya naye kazi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -