Saturday, January 16, 2021

PONGEZI AZAM ILA EPUKENI MAKOMANDOO

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA WINFRIDA MTOI

KWA muda mrefu klabu ya Azam FC ilikuwa inatamani mechi zake za nyumbani zinazohusisha timu za Simba na Yanga, kuchezwa katika uwanja wao wa Azam Complex, lakini kwa misimu kadhaa ilikuwa ikishindikana.

Sababu kubwa iliyokuwa ikitolewa na Shirikisho la Soka nchini ‘TFF’, kushindwa kuutumia  ni hali ya usalama  kutokana na timu za Simba na Yanga kuwa na mashabiki wengi kulinganisha na uwezo wa uwanja huo  ambao  una uwezo wa kubeba mashabiki 7,000-10,000.

Hata hivyo, Azam hawakukata tamaa kwani waliendelea kupambana na kushughulikia mapungufu yanayodhaniwa ni kikwazo kwao cha kutopewa nafasi ya kutumia uwanja wao kwa mechi za timu kubwa.

Licha ya kwamba huko nyuma Simba na Yanga ambazo hazina viwanja, ziliwahi kuutumia uwanja huo kwa mechi zake, lakini rasmi msimu huu TFF imeamua kuruhusu Azam kucheza kila mchezo wao wa nyumbani katika uwanja wa Azam Complex uliopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Katika mechi yao waliyocheza na Simba juzi kwa kutumia uwanja wao wa nyumbani na kutoka suluhu, kiingilio cha chini kilikuwa Sh 6,000.

Kulingana na utaratibu uliokuwepo juzi, ilionyesha ni jinsi gani Azam walikuwa wanataka kuudhihirishia umma na wapenda soka kwamba, kilio chao kilikuwa sahihi cha kutaka kuruhusiwa kutumia uwanja wao.

Baada ya TFF kutangaza kwamba mechi ya Simba itachezwa Chamazi, baadhi ya watu walikuwa na shaka na kutoridhishwa na kitendo hicho kwa madai ya ufinyu wa eneo hilo na uwezo wa kuhudumia idadi kubwa ya mashabiki.

Lakini mambo yamekwenda tofauti na matarajio ya wengi, kwani utaratibu uliokuwepo wa kuimarisha usalama, ulizidi hadi ule unaotumika kwenye Uwanja wa Taifa kwani kila kitu kilikwenda katika mpangilio na mashabiki waliingia kulingana na idadi  iliyopangwa.

Ule ujanja ujanja tunaoshuhudia katika viwanja vingine haukuwepo, pia uwepo wa eneo kubwa kuegesha magari, iliwaondolea usumbufu mashabiki waliofika na usafiri wao ambao kwenye viwanja vingine ikiwamo Uhuru wanalazimika kuwalipa vijana wawalindie vyombo vyao vya usafiri.

Ifahamike kuwa kila mtu anapotoka nyumbani kwenda kutazama mpira anahitaji kupata burudani na si karaha, hivyo nawapongeza Azam kwa kuonyesha mfano wa jinsi shabiki au mdau wa soka anavyotakiwa kuhudumiwa.

Ila sasa, siku zote katika msafara wa mamba na kenge wapo, licha ya kwamba walinzi wa Azam, TFF na Jeshi la Polisi walikuwa wamejipanga pande zote kuhakikisha hali ya usalama inakuwa shwari, wale watu waliozoea ubabaishaji katika viwanja vingine nao walitaka kuharibu uhondo huo.

Hawa ni wale wanaojiita makomandoo wa timu, ambao kwenye mechi kama hizi wamezoea kuingia uwanjani kwa njia zao wanazojua wao,  walitaka kuchafua hali ya hewa kwa kuanza kusumbua watu wengine ili kupata mwanya  wa kufanya yao.

Utaratibu unajulikana kuwa kila anayeingia uwanjani lazima awe amelipia kiingilio na utambulisho wake ni tiketi, au kwa wale watu maalumu wana vitambulisho vyao na vinaelekeza ni eneo gani anatakiwa kukaa na kama haelewi inabidi aelekezwe na mtu aliyepo getini.

Watu hawa tabia yao ni kujichanganya kwenye milango  na kukagua tiketi au vitambulisho,  lakini ukiangalia hawatambui kazi  wanayotakiwa kufanya na badala yake wanashindwa kuwaelekeza watu kwa utaratibu na kuanza kupigishana nao  kelele kitendo  ambacho ni kero.

Ijulikane kuwa unapopewa dhamana ya kusimama mlangoni  hasa katika sehemu ambazo watu wamelipa fedha zao  kwa lengo la kupata burudani, unatakiwa kuwa makini katika kuwaelewesha na si kutumia lugha kali.

Kutokana na hali hiyo, Azam wanatakiwa kujiepusha na watu wa aina hii kwani wataharibu kile walichokipanga cha kuufanya uwanja wao kuwa wakimataifa na kuendeshwa katika utaratibu wa pekee.

Tunajua uwanjani kuna askari wa Jeshi la Polisi, walinzi wa TFF na uwanja husika, kwanini makomandoo wapewe nafasi ya kuwakera mashabiki ambao wanalipa viingilio vyao.

Kama miongoni mwa watu waliofika kutazama mechi hiyo na kupata nafasi ya kuzunguka maeneo yote watu wanapoingilia, hakuna vurugu za ajabu, ila kasoro ni hiyo ya watu wachache wanaojiita makomandoo waliotaka kuharibu utamu wa mambo.

Mechi ya Simba tayari imepita, tunaamini katika mchezo mwingine  dhidi ya Yanga,  kutakuwa  na maboresho zaidi na kuondoa kasoro zilizojitokeza  hasa kuondoa watu wasiohusika kwenye mageti.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -