Sunday, October 25, 2020

PONGEZI KWA TIMU YA KRIKETI U-19, ENDELEENI KUKAZA BUTI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA WINFRIDA MTOI


TIMU ya kriketi Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 19, iliyokuwa inashiriki michuano ya Daraja la Pili Afrika (Division II), nchini Afrika Kusini, imefanya vizuri kwa kufanikiwa kutinga hatua ‘Division I.

Katika michuano hiyo, iliyoanza Agosti 17, mwaka huu na kumalizika juzi, timu ya Tanzania ilifanikiwa kufika fainali na kukutana na Msumbiji na kuibuka kidedea kwa kushinda kwa mikimbio 215-140.

Tanzania ilianza vema michuano hiyo  na kushinda mechi nne mfululizo,  walianza kuichapa Swaziland kwa mikimbio 262-99, mechi ya pili  walicheza dhidi ya Rwanda na kushinda  kwa mikimbio 134-114

Michezo mingine walishinda dhidi ya Botswana kwa mikimbio 161-136 na mchezo wa nne waliifunga Nigeria kwa mikimbio 137-121.

Pamoja na mafanikio ya timu hiyo, pia Tanzania imetoa mchezaji bora wa mashindano ambaye ni Aahil Jasan.

Kutokana na matokeo hayo, Tanzania inaungana na Nigeria, Kenya, Uganda, Namibia, Sierra Leone kushiriki michuano ya Division 1, inayotarajia kufanyika Aprili mwakani.

Endapo timu hiyo itafanikiwa kufanya vizuri katika michuano hiyo ya mwakani, itakuwa imekata tiketi ya kucheza Kombe la Dunia itakayofanyika  mwaka 2020, kwa sababu kati ya timu hizo, zinatakiwa mbili pekee.

Ukiangalia kwa mtiririko wa matokeo ya mechi za Divison II, Tanzania ina nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia, kinachotakiwa ni kutobweteka na kuendelea na maandalizi.

Viongozi wa Chama cha Kriketi Tanzania (TCA) pamoja na wadau wengine wa mchezo huo ni wakati sasa wa kuongeza nguvu kwenye timu, hasa katika kupata mechi nyingi za kirafiki za kimataifa.

Pia kuongeza wachezaji wengine ambao watakuja kuziba nafasi za wale watakaokuwa wamezidi miaka chini ya 19, inapofika mwakani.

Naamini kufanya vizuri kwa timu ya Tanzania kumechangiwa zaidi na marekebisho waliyofanywa na TCA, hasa upande wa ufundi kwa kuleta kocha mpya mwenye viwango vya kimataifa.

Mapema mwaka huu, kriketi walimleta kocha Peshotan Mehta, raia wa India, ambaye ana uwezo mkubwa wa mchezo huo kutokana na asili ya nchi anayotoka iko juu katika kriketi duniani.

Kocha huyo ndiye aliyeanza kukisuka upya kikosi hicho kwa kufanya mchujo wa wachezaji mbalimbali na matunda yake yameonekana.

Nawapongeza viongozi wa kriketi Tanzania kwa mafanikio hayo, lakini rai yangu kwa wanakriketi ni kuendelea kumshikiria mwalimu huyo ili aweze kuendeleza programu iliyokuwa imeanza ya kuibua vipaji na kuendeleza kriketi nchini.

Matokeo yaliyopatikana mwaka huu, ilikuwa ni nadra kuyapata kwa sababu tumeshuhudia timu za taifa za kriketi kabla ya ujio wake, zikifanya vibaya katika michuano mbalimbali.

Hivyo basi, kuvuka hatua ya Division I kwa Tanzania, nafasi ambayo ilikuwa inatafutwa kwa muda mrefu ni mafanikio makubwa, lakini kila mwenye jukumu lake anatakiwa kufahamu kuwa bado kazi ni  kubwa, ili kufuzu Kombe la Dunia.

Inafahamika kriketi ni moja ya michezo inayoitangaza sana Tanzania kutokana na kushiriki michuano mingi ya kimataifa kuliko vyama vingine vya michezo ya ndani.

Pia umekuwa ni mchezo wenye ligi nyingi zinazoshirikisha wachezaji wa rika tofauti, kuanzia miaka nane na kuendelea, hivyo basi, juhudi hizo zinatakiwa kuendelezwa.

Nafahamu kuna changamoto nyingi  ambazo chama cha kriketi kinapitia, lakini jambo la msingi ni kuwa na misimamo ya kuhakikisha hawayumbishwi na watu wasiopenda maendeleo ya michezo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -