Thursday, December 3, 2020

POULSEN KUMRITHI MKWASA T/STARS

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA MWANDISHI WETU


MSHAURI wa ufundi timu za vijana nchini Tanzania, Kim Poulsen, huenda akarejea kwenye kibarua chake cha zamani cha kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kim anapewa nafasi ya kumrithi Charles Boniface Mkwassa na kwamba kocha wa muda wa timu hiyo, Salum Mayanga, atakuwa msaidizi wake.

Kim ambaye anafundisha soka kwa mwaka wa 30 sasa tangu alipoanza kazi hiyo mwaka 1987, anatarajiwa kutangazwa hivi karibuni kama kocha wa timu hiyo.

Habari za ndani ambazo BINGWA limezipata kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zinasema kuwa tayari mazungumzo na kocha huyo yameshafanyika juu ya nafasi hiyo.

“Ni kweli kuna mpango wa kumpa timu Kim na hili limefikiwa baada ya kujadili masuala kadhaa, tunaamini Kim anaijua vyema Stars, lakini pia alishakuwa kocha na sasa ndiye mshauri wa ufundi wa timu za vijana, hivyo atakuwa anafahamu vyema namna bora ya kuijenga timu,” alisema mtoa habari wetu ambaye hata hivyo aliomba asijatwe jina kwa kuwa yeye si msemaji wa TFF.

Alipotafutwa, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo na zaidi alisema atatuma taarifa lakini taarifa aliyoituma baadaye ilihusu mambo mengine.

Katika hatua nyingine, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limemteua Rais wa TFF, Jamal Malinzi, kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya soka ya Fifa kwa miaka minne ijayo.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyotolewa na Ofisa habari wa Shirikisho hilo jana,  Malinzi anaungana na wajumbe wengine kwenye kamati inayoongozwa na Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa  ambaye ni Rais wa Shirikisho la Soka la Bara la Asia, ina majukumu ya kusimamia mipango ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani kote.

Huu ni mfululizo wa Tanzania kupata nafasi katika vyombo vikubwa vinavyoendesha soka; Fifa na CAF. Mwishoni mwa mwaka jana, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilimteua Rais Malinzi kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati maalumu inayoongozwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou, ya kuboresha mfumo wa uongozi wa CAF.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -