Wednesday, November 25, 2020

PRINCE AMIGO AWAPONDA WANAOJIITA WAFALME WA TAARAB

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA KYALAA SEHEYE,

HAKUNA ubishi kuwa baada ya Mzee Yusuph kuachana na taarab, wengi waliamini muziki huo unaweza kuyumba, wakijua hakuna ambaye angeweza kuvaa viatu vyake.

Katika kuonyesha wapo wanaoweza kuziba pengo lake, baadhi ya waimbaji waliibuka ghafla na kujipa jina la Mfalme wa Taarab, alilotamba nalo Yusuph hadi anastaafu muziki huo.

Mwisho wa siku, waimbaji kibao kila walipopanda jukwaani, walijinadi kuwa wao ndio wafalme wa taarab nchini.

Lakini, kitendo hicho kinaonekana kuzidi kuudidimiza muziki huo, kwani wale wanaojiita wafalme wa muziki huo wamebaki kuvaa joho la Mfalme wa Taarab, Mzee Yusuph, badala ya kubuni mitindo yao.

Kwa kufahamu hilo, BINGWA lilimtafuta mkali wa muziki wa taarab nchini aliyefanya kazi na Mzee Yusuph kwa muda mrefu ndani ya Jahazi Modern Taarab, Abubakari Soud ‘Prince Amigo’ na kufanya naye mahojiano juu ya hali ilivyo katika muziki huo kwa sasa.

Katika mahojiano hayo, Prince Amigo anasema kuwa, anawashangaa sana wanaoutaka ufalme wakati hawajatokea katika ukoo wa kifalme.

“Mfalme Mzee Yusuph hakuacha kazi hii ghafla, ni jambo alilolipanga kwa miaka mingi, ila siku na wakati ilikuwa bado, alituweka na kutupa misingi mapema sana na hivyo nina imani Jahazi haiwezi kufa wala kuporomoka na itazidi kuwa juu kuliko hata inavyodhaniwa,” anasema.

Amigo ni miongoni mwa vijana ambao ni zao la Mzee Yusuph na ndiyo maana alipewa jina la Prince, akimaanishwa mtoto wa mfalme na wadau wengi wa taarabu wanaamini kijana huyo ameuvaa ufalme huo kutokana na uwezo wake awapo jukwaani.

“Baba yangu kimuziki ambaye ndiye Mfalme mstaafu, mara kwa mara alikuwa akiniusia na kuniomba hata kama ataacha kazi, nihakikishe ninaikuza bendi kwa kufuata misingi na maadili kama alivyokuwa anafanya yeye.

“Nami ndivyo ninavyofanya, nina imani tutafika, kama watu wananitabiria kuwa Mfalme, mimi sina wasiwasi kwa sababu ni mtoto wa Mfalme na ufalme ni kitu cha kurithishana, hiyo inajulikana, ndiyo maana sikupenda kujitangaza, nilisubiri nitangazwe,” anasema Prince Amigo.

Pia mkali huyo anawashangaa wapinzani wao kuacha kuimba taarabu ambayo ni muziki wa wastaarabu na ulio na maadili na badala yake kuingiza matusi katika nyimbo, akiamini huko ni kujiua wenyewe.

“Nadhani hakuna asiyejua, Jahazi imetoa wanamuziki wengi hapa nchini, sasa hao ndio wamegeuka na kuimba matusi, sasa sijui wamefunzwa wapi, kwani Mfalme katu hakutufundisha hivyo, alitufunza kutoa burudani na kufikisha ujumbe. Hata ukiangalia wimbo tulioanza nao bila Mfalme wa Nataka Jibu ni ujumbe tosha, katu hauna matusi,” anasema.

Kwa upande wake, mpiga kinanda mkongwe wa Jahazi, Ally Juma ‘Ally J’, alisema bendi yao hiyo ilikuwa inawapa tumbo joto viongozi na waimbaji wa bendi nyingine kutokana na umahiri na uwezo wake na ndiyo maana wakaamini itakufa baada ya kuondoka Mzee Yusuph.

“Mimi nilipokuwa nje ya Jahazi nilikuwa najua wazi kuwa hii ni bendi bora na hakuna asiyejua na hata alipoondoka Mfalme, nilikuwa nikijua haitakufa kwasababu hakukurupuka, ni kitu alichokuwa amekipanga, hivyo aliacha mipango thabiti,” alisema.

Prince Amigo na Jahazi yao kwa sasa wapo katika maandalizi ya kumbukumbu ya miaka 10 ya bendi yao hiyo tangu kuanzishwa kwake, ambapo tukio hilo litafanyika ndani ya Ukumbi wa Dar Live, Mbagala, jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -