Saturday, October 31, 2020

PRISONS KUWAKABILI WABABE WA SIMBA LEO 

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WINFRIDA MTOI

LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea leo kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja tofauti, ambapo maafande wa Tanzania Prisons watavaana na wababe wa Simba, Mbao FC, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,  Mwanza.

Katika msimamo wa ligi hiyo kabla ya mechi za jana, Mbao walikuwa wanaongoza kwa pointi 10 baada ya kucheza michezo tano, ambapo wameshinda mara tatu, kupata sare moja na kufungwa mmoja.

Kwa upande wa Prisons iliyopo nafasi ya 16 ikiwa na pointi tano, imeshuka dimbani mara tano na kushinda mchezo mmoja, kupata sare mbili na kufungwa mara mbili.

Akizungumza na BINGWA jana, kocha mkuu wa Prisons, Abdallah Mohamed, alisema wamejiandaa kupata pointi tatu katika mchezo huo na hawawahofii wapinzani wao kwa sababu ya kuifunga Simba.

“Mbao wamewafunga Simba lakini si Tanzania Prisons, sisi tumekuja jijini Mwanza kwa lengo la kutafuta pointi tatu, hatuwezi kuuhofia mchezo kwa kuwa tumejiandaa,” alisema Mohammed.

Naye kocha wa Mbao FC, Amri Said, alisema jambo la muhimu ni mashabiki kujitokeza kuendelea kuisapoti timu yao kama walivyofanya katika michezo iliyopita.

Katika michezo mingine itakayopigwa leo, Ndanda FC itavaana na Stand United katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara, wakati Mtibwa Sugar watakuwa ugenini kumenyana na African Lyon kwenye dimba la Uhuru, Dar es Salaam.

Mtibwa wanaoshika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi, watashuka dimbani wakiwa wametoka kupoteza mchezo wao uliopita kwa kufungwa mabao 2-0 na Ndanda FC, mjini Mtwara, wakati wapinzani wao African Lyon wametoka kushinda mabao 3-2 dhidi ya Singida United.

Stand United ambao watakuwa wageni wa Ndanda, wametoka kupoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Yanga kwa kufungwa mabao 4-3 na kuchapwa 2-0 na KMC.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -