Sunday, November 29, 2020

RAGE AWASHUKIA YANGA KESI YA FAKHI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

WAKATI Simba ikitarajia kujua hatima yao dhidi ya beki wa Kagera Sugar, Mohammed Fakhi, waliyemkatia rufaa kwenye kamati ya saa 72, Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo ya Msimbazi, Ismail Aden Rage, ameishukia Yanga kwa kuwaambia ‘pilipili ya shamba inawawashia nini’.

Kauli hiyo ya Rage inakuja siku moja baada ya Yanga kutangaza kwamba watakwenda Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuchunguza taarifa za waamuzi na makamisaa kuhusu rufaa hiyo ya Simba.

Lakini Rage akizungumza na BINGWA jana, aliijia juu Yanga na kusema inapaswa kuiacha kamati hiyo ifanye kazi yake ipasavyo kwani waliopaswa kulalamika ni Kagera Sugar na si wao.

“Hivi pilipili usioila inakuwashia nini? Yanga inawahusu nini? Yule mwamuzi ni wa Simba na Kagera. Sasa kinachowasumbua Yanga sijui ni kitu gani, wanapaswa kuacha kamati itimize majukumu yake,” alisema Rage.

Rage alikwenda mbali zaidi kwa kuwataka Yanga kwenda popote wanapotaka kwa kuwa ni haki yao kisheria ila aliwakumbusha watakapothubutu kwenda mahakamani wajiandae kushushwa daraja.

“Takukuru, TCRA unaweza kwenda kwa kuwa haki ya kisheria inakuruhusu, ila utakapothubutu kwenda mahakamani ujiandae kushushwa daraja,” alisema.

Alimaliza kwa kuwataka Yanga kukaa pembeni msimu huu kwa kuwa miaka mitatu waliokuwa wakipokezana na Azam hawajawaza kufanya lolote la maana kwenye michuano ya kimataifa.

“Yanga wawaache wanaume (Simba) wafanye mambo yao msimu huu wakapeperushe vema bendera ya Taifa, yaani miaka yote mitatu waliokuwa wakishiriki wamekuwa wakipanda ndege mara moja na kurudi, wawaache Simba na rekodi zao za kimataifa,” aliongeza.

Wakati Rage akiyasema hayo, naye Katibu wa Baraza la Wazee Simba, Abdul Sharifu, alisema rufaa yao imefuata misingi yote hivyo hawana wasiwasi na wanaamini watapewa pointi tatu muhimu.

“Waacheni Yanga wapige kelele, sisi wala hatuna mashaka tunajua leo tunapewa pointi zetu tatu, kwa kuwa rufaa yetu dhidi ya Fakhi ni halali na kweli alikuwa na kadi tatu za njano,” alisema.

Simba kwa sasa wapo kileleni kwa pointi 58, huku mahasimu wao Yanga wakifuatia nafasi ya pili wakiwa na pointi 56, huku wakiwa na kiporo cha mechi moja mkononi. Kama Simba watashinda rufaa hiyo ya kupewa pointi tatu na mabao mawili kama taratibu zinavyosema, basi kikosi hicho cha Msimbazi kitakuwa na jumla ya pointi 61 na kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -