Saturday, October 31, 2020

RAIS BARCA ARIDHISHWA NA KIKOSI CHAO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

BARCELONA, Hispania


 

RAIS wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, ameelezea kuridhishwa na kikosi chake ambacho ni mabingwa wa La Liga, licha ya kuendelea kuhusishwa na staa wa Manchester United, Paul Pogba.

Mfaransa huyo ndiye aliyeiongoza Manchester United katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu England na akaweza kufunga bao kwa mkwaju wa penalti ambao uliwasaidia kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leicester City wakiwa katika dimba lao la Old Trafford.

Hata hivyo, mara baada ya mchezo huo, Pogba alitikisa kwenye vyombo vya habari kutokana na kauli tata aliyoitoa akisema kuwa angeweza kulimwa faini kama angeweza kuzungumza chochote kuhusu klabu hiyo.

Uhusiano kati ya Pogba na kocha wake,  Jose Mourinho, uliingia kwenye msukosuko msimu uliopita, baada ya kiungo huyo kuwekwa benchi katika michezo yote miwili ya Ligi ya Mabingwa ambayo walitupwa nje na  Sevilla.

Mpaka sasa mabingwa wa Serie A, Juventus bado wanahusishwa kumtaka tena staa wao huyo wa zamani, huku  Barca nao wakiripotiwa kuvutiwa naye, licha ya kuwa wameshasajili  viungo wengine, Arturo Vidal na Arthur, kabla ya msimu ujao haujaanza kutimua vumbi ambapo Jumamosi watakuwa nyumbani wakiivaa, Deportivo Alaves.

Akizungumza juzi mara baada ya mchezo wao wa usiku wa kuamkia jana ambao waliondoka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Boca Juniors na kufanikiwa kutwaa Kombe la Joan Gamper, kigogo huyo alisema kwamba kwa sasa ameridhika na kikosi chake licha ya kuhusishwa na nyota wengine.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -