Wednesday, October 28, 2020

RAIS MAGUFULI HAKUELEWEKA KUHUSU MCHEZO WA ‘POOL’

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA GRACE HOKA


KUMEKUWAPO na dhana kuwa mchezo wa ‘pool’ (Pooltable) ambao hupendwa na watu wa rika zote, wakiwamo vijana, wanaume, wanawake na wazee, hivi sasa umeshuka tofauti na zamani.

Miaka miwili ya nyuma mchezo huo ambao huchezwa sana na vijana ulishika kasi, hali iliyopelea kuanza kuchezwa asubuhi hadi usiku mkubwa.

Mbali na kuchezwa katika pande zote za Tanzania, mchezo huo umekuwa ukitoa ajira kwa watu mbalimbali hali liyowafanya vijana wengi kujikwamua kiuchumi.

Tofauti na kujikwamua kiuchumi pia mchezo wa ‘Pooltable’ umekuwa ukiwakutanisha vijana hasa wale ambao hawana ajira rasmi, wamekuwa wakikutana wakicheza mchezo huo huku wakipata burudani pamoja na kupanga  mambo mbalimbali ya maisha yao ya kila siku.

Watu wengi hawafahamu kuwa mchezo wa Pooltable ni moja ya michezo ambayo  huingiza fedha nyingi, ikiwa  ni pamoja na kufanya watu kuishi maisha mazuri hapa  nchini kwa kujipatia mahitaji yao muhimu.

Mchezo wa Pooltable ndio mchezo pekee ambao hufaidisha makundi matano katika jamiii kwa wakati mmoja, yote hupata fedha kupitia mchezo huo.

Makundi hayo yanayofaidika ni pamoja mnunuzi wa meza ya mchezo huo, kwenye sehemu ambazo meza hiyo huwekwa, msimamizi wa meza, muuzaji ambao ni kampuni ya Kenice Funiture Transpot, pia Serikali inalipwa kutokana na tozo ya kodi.

BINGWA hivi karibuni lilifanya mahojiano na Meneja mkuu wa kampuni ya Kenice, Eustace Masaki, ambapo ndio watengenezaji wakuu wa meza na vifaa vinavyotumika katika kucheza mchezo huo.

Mbali na kutengeneza vifaaa vya mchezo huo, kampuni hiyo pia imekuwa ikidhamini mashindano mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika hapa nchini kuanzia ngazi ya mikoa hadi Taifa.

Katika mahojiano hayo Meneja huyo alizungumza mambo mengi, mojawapo ni kusisitiza mashindano ya pool kuendelea kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Alisema kuwa mchezo huu bado upo juu,  unachezwa sana katika sehemu mbalimbali za nchi, katika mikoa yote ya Tanzania Bara na visiwani.

Masaki anasema kuwa mchezo wa Pooltable umekuwa ukitoa ajira kubwa sana kwa Watanzania, kwani makundi mbalimbali yamekuwa yakifaidika sana na mchezo huo.

Alisema kuwa watu wengi wanadhani kuwa mchezo huo hivi sasa umekuwa hauchezwi kama zamani, kitu ambacho amedai kuwa si kweli isipokuwa kauli ambayo ilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe  Magufuli, kuwa ni marufuku kucheza Pooltable wakati wa kazi.

Alisema kuwa kauli ile ya Rais watu hawakuilewa, alikuwa na maana kwamba  mchezo wa Pooltable usichezwe wakati wa kazi na si kuupiga marufuku kabisa.

Alisema kuwa kauli hiyo ya Rais Magufuli haikueleweka vizuri kwa wananchi, kwani hakukataza starehe isipokuwa alikataza mchezo huo kuchezwa wakati wa kazi.

Kauli hiyo iliathiri kidogo mchezo huo wa pili lakini kwa sasa umerudi kama zamani.

“Hata watendaji wa chini walikuwa wakitoa kauli mbalimbali kutaka mchezo  huo kuchezwa, lakini hawakumwelewa Rais kauli aliyoitoa haikumaanisha kwamba mchezo huo usichezwe ila uchezwe wakati ambao sio wa kazi,” alisema.

Alisema kuwa wao ndio walipelekea mchezo wa Pooltable kupenda sana hapa nchini, kwani walifanikiwa kuutangaza ikiwa ni pamoja na kusapoti chama cha mchezo huo.

Alisema kwamba wamepanga kufanya mambo mengi mwaka 2017 ikiwa ni pamoja na kurudisha mashindano mbalimbali ya mchezo huo, kuongozeza idadi ya uzalishaji wa vifaa vya mchezo huo hapa nchini.

Alisema kuwa wao kama watengenezaji wa vifaa vya mchezo huo hapa nchini wamekuwa wakifanya harakati za kuutangaza mchezo huo katika nchi mbalimbali za Afrika.

Alisema kuwa wao wamekuwa wakipeleka vifaa vya mchezo huo katika nchi za Msumbiji, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zambia na Kenya ambako ndiko yaliko makao makuu wa  kampuni hiyo.

Alisema kuwa wazo la kuanzisha kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya mchezo huo lilitokea nchini Afrika Kusini mwaka 1998 baada ya kufika nchini, menejimenti iliamua kuanza kuutangaza hapa nchini ikiwa ni pamoja na kutengeneza vifaa vya mchezo huo.

“Lengo letu tunataka hadi kufikia mwaka 2018 mchezo wa pooltable uchezwe na kila mtu,” alisema Meneja huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -