Thursday, December 3, 2020

Rayvanny amejitofautisha na Diamond

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA HAPPYGLORY URASSA,

JINA la Msanii Raymond, maarufu kama Rayvanny, limechomoza kwa kasi katika muziki wa Bongo Flava hapa nchini. Ni msanii aliyeibuka kwa kasi kubwa na kuteka hisia za wapenzi wengi wa muziki huo kutokana na aina yake ya uimbaji pamoja na ujumbe mzuri katika tungo zake.

Wimbo wake wa Natafuta kiki, ulimtambulisha vizuri kwenye fani ya muziki huo akiwa chini ya lebo maarufu ya muziki hapa nchini hivi sasa ya WCB, lakini kabla wimbo huo haujasahaulika masikioni mwa mashabiki wa muziki, alitoka na wimbo wa Kwetu, ambao kwa kiasi kikubwa ulichangia kulipaisha jina la msanii huyo.

Kipaji  na uwezo wa msanii huyu siyo jambo la kuuliza kwa sasa, kwani uwezo wake umejidhihirisha ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, kwani kwa sasa amekuwa msanii pekee aliyesainiwa na WCB, kutajwa kuwania tuzo kubwa za MTV Mama, zinazofanyika huko Johannesburg, Afrika Kusini, mwishoni mwa mwezi huu.

Raymond pia anawania tuzo ya African Entertainment USA, zinazo fanyika huko Marekani, baadaye mwaka huu.

Tofauti na wasanii wengine walioko chini ya WCB, msanii huyu amedhihirishia Watanzania kwamba yeye siyo wa mchezo mchezo, kwani nyimbo zake zote zimefanikiwa kuwakamata vilivyo mashabiki, ukiwemo wimbo ambao ameutoa akishirikiana na nguli Diamond Platinum wa Salome, ambao unaendelea kufanya vyema kwenye chati za muziki hapa nchini na Afrika Mashariki.

Ni jambo lililowazi kwamba uwezo wa msanii huyo ndio unaombeba na hasa kumvutia bosi wa WCB, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ kiasi cha kuamua kumsajili kwenye lebo yake na pia kufanya naye kazi kwa ushirika wa moja kwa moja.

Rayvanny amejipambanua kwa sauti na amejiweka tofauti na Diamond, hivyo hata kama wakifanya kazi pamoja wanaonekana kuwa ni wasanii wawili tofauti, na hii ni karata yake muhimu kwa wasaanii wote walio chini ya WCB, ambao wengine wamekuwa wakiimba kama Diamond, kwa maana ya kumuiga bosi wao kwa sauti na hata uchezaji, jambo ambalo linawatesa.

Mashabiki wengi wa muziki wamekuwa wakimsifia sana Rayvanny kutokana na ukweli kwamba yeye amekuwa tofauti na wengine. Wengi wamewalalamikia wasanii wanaoingia WCB kutokana na kukosa ubunifu na kujikuta wakiimba chini ya kivuli cha bosi wao, Diamond kwa kumuiga kila kitu.

Rayvanny ana hasira ya mafanikio, na hii inamfanya kujituma zaidi katika kutunga nyimbo nzuri zenye ujumbe, lakini pia ambazo zitatoa burudani murua kwa mashabiki wa muziki hapa nchini.

“Najua mafanikio hayaji hivihivi, lazima niweke jitihada za dhati, najituma hasa katika kuandaa kazi zangu na zaidi ya hapo najipanga kuwa tofauti kila wakati ili kuhakikisha nikitoka watu wanaona tofauti yangu na wasanii wengine,” anasema Rayvanny.

Tofauti na wasanii wengine wengi wachanga wanaotoa wimbo mmoja na kuanza dharau na kejeli kwa watu waliowatangulia kwenye muziki, Rayvanny amekuwa mtu wa kujifunza na kusikiliza, ameziacha kazi zake nzuri anazozifanya zimpe umaarufu zaidi ya ‘kiki’ zisizokuwa na tija  kwenye mitandao ya kijamii.

Alivyotoa wimbo wake wa Kwetu kama ilivyo wa wasanii wengi kupotea baada ya wimbo mmoja, watu hawakutilia shaka uwezo alionao msanii huyo, kwani aliuonyesha utofauti wake na wasanii wengi waliopita na kuthibitisha hilo kwenye wimbo wake uliofuatia.

Kuingia WCB ndiyo ilikuwa tiketi ya mwanzo wa mafanikio ya msanii huyo alipopata nafasi na aliitumia na bado anaitumia vizuri. “Ukipata nafasi lazima uitumie vizuri, nipo hapa nashukuru kwa nafasi ninayoipata na ninajituma kuhakikisha sipotezi nafasi hii,” anasema.

Kwa sasa Rayvanny ndiye msanii anayechipukia anayeangaliwa zaidi na vyombo vingi vya habari Afrika, kwani ni kati ya wasanii wengi wanaochipukia kwenye tasnia ya muziki wa bongo flava. Tumeona akitajwa kuwania tuzo kubwa akiwa  ndiye msanii wa kwanza chipikizi kwa Tanzania kuingia kwenye tuzo za kimataifa akiwa na nyimbo mbili tu.

Kwa sasa mkali huyo anatamba na wimbo alioshirikiana na Diamond wa Salome, ambao kwa sasa wimbo huo ambao una wiki tatu tu umepata watazamaji zaidi ya milioni 4 kwenye mtandao wa Youtube na hivyo kuendelea kulipaisha jina la Rayvanny katika medani ya muziki kimataifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -