Saturday, January 16, 2021

Redknapp aichuria Man Utd kukosa ubingwa

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

KOCHA wa zamani wa Tottenham, Harry Redknapp, ameiondoa Manchester United katika mbio za ubingwa akiamini tumaini lao limetoweka, baada ya mwishoni mwa wiki kushindwa kuifunga Burnley Old Trafford.

Akizungumza kupitia mtandao wa BT Sport, kocha huyo alisema kwamba anavyoamini taji lipo mbali sana na uwezo wa Mashetani Wekundu, haijalishi tofauti ya pointi ngapi baina yao na vinara wa ligi, Manchester City.

Jose Mourinho, alikereka kuishuhudia timu yake ikiambulia suluhu katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Burnley iliyopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Old Trafford.

United wameweka rekodi ya ligi kuu kwa mashuti mengi golini tangu rekodi za Opta zilipoanzishwa msimu wa 2003/04, lakini bado hawakuweza kufunga bao.

Klabu hiyo inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu, pointi nane nyuma ya vinara na wana shughuli pevu kurudi kwenye mbio za ubingwa.

Lakini Redknapp anaamini kwamba, hata kama wangekuwa na tofauti ya pointi tatu kutoka pale wanapotaka kuwa bado wasingekuwa na nafasi ya kutwaa taji.

“Hawawezi kushinda, hawana ubora wa kutosha. Naliitazama timu ya Man United, nilipenda kwenda pale miaka michache iliyopita nikiwa na timu na kucheza dhidi yao,” alisema kocha huyo.

“Nilikuwa nikitembea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, nikiwatazama na walikuwa tishio, hofu ya kifo kabisa.

“Lakini kucheza dhidi yao kwa sasa, ni timu duni isiyoweza kushinda taji la Ligi Kuu kwa maoni yangu,” aliongeza kocha huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -