Saturday, October 31, 2020

REKEBISHA, POVU, NYIMBO ZINAZOIFUFUA TWANGA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU

BENDI ya muziki wa dansi nchini ya The African Stars International ‘Twanga Pepeta’, imeachia nyimbo mpya mbili wiki iliyopita na zimeanza kufanya vizuri.

Nyimbo hizo mbili ambazo moja iitwayo Povu imetungwa na mshindi wa Shindano la Bongo Star Search (BSS), mwaka 2011, Haji Ramadhani ‘Haji BSS’, wakati ule mwingine wa pili uitwao Rekebisha umetungwa na Msafiri Diouf.

Waimbaji walioimba katika wimbo huo wa Povu ni Haji BSS mwenyewe, Kalala Junior, Diouf na mwimbaji mpya wa bendi hiyo, Joshua Mwasasunda ‘Piano’.

Huku ule wa Rekebisha ukipambwa zaidi na chipukizi kama Fatuma Kalumbu ‘Fetty’, Piano, Zubeiri Kibenten na wakongwe kama Diouf na Kalala.

Kwanza ni muda mrefu Twanga walikuwa kimya bila kutoa nyimbo, lakini staili ya nyimbo hizo ni kitu ambacho kilikuwa kikikosekana.

Mara ya mwisho Twanga kutoa wimbo ambao una maudhui au staili ya bendi hiyo ilikuwa ni mwaka 2012 baada ya kurejea kwa Kalala akitokea Mapacha Watatu na kibao hicho kiliitwa Nyumbani ni Nyumbani.

Lakini kabla ya hapo nyimbo ambazo zilikuwa zinaendana ama zina utambulisho wa bendi hiyo ya Twanga Pepeta, ilikuwa kwenye albamu ya Dunia Daraja ambayo ilitungwa na Charles Gabriel ‘Chalz Baba’, ambaye baadaye alitimkia Mashujaa Band mwaka 2012.

Katika albamu hiyo kulikuwa na nyimbo nyingine kali kama Kauli na Kiapo cha Mapenzi ambazo zilitungwa na Salehe Kupaza na kufanya vizuri na zaidi ya yote zilikuwa kwenye staili ya bendi hizo ambazo zimezoeleka hata kwa mashabiki wa dansi wakisikia wanajua hao ni Twanga Pepeta.

Nyimbo za aina hiyo zilikosekana kwa muda Twanga Pepeta na kufanya muziki wa dansi kuonekana umeshuka, lakini ni kukosa tungo mpya nzuri kama ambavyo mashabiki wamezoea kusikia.

Nyimbo hizo za Povu na Rekebisha ambazo kabla ya kuachiwa zilikuwa zimeanza kupigwa kwenye maonyesho mbalimbali ya bendi hiyo, ikiwamo lile la kila Jumamosi katika Ukumbi wa The Jonz.

Hizo ni nyimbo ambazo zimepokelewa kwa mikono miwili na mashabiki na wadau mbalimbali wa muziki wa dansi kutokana na staili yake kuwa ni ile ambayo imezoeleka kutumiwa na bendi hiyo.

Pamoja na nyimbo hizo pia kurejea kwa Chalz Baba nako kumeongeza chachu ya hamasa kwa waimbaji wa bendi hiyo na mashabiki.

Chalz Baba ni mwimbaji mwenye uwezo wa hali ya juu na kipaji kikubwa cha kutunga nyimbo nzuri ambazo staili yake imezoeleka na mashabiki wa Twanga na wale wa muziki wa dansi.

Akizungumza na Mtanzania Digital hivi karibuni, Chalz Baba alisema amekwishaandaa nyimbo mbili ziitwazo Moyo Koma na Wakala.

Tayari nyimbo hizo zimeanza kufanyiwa mazoezi zikitarajiwa kuwamo kwenye albamu mpya ya bendi hiyo na Onyesho la Miaka 20 ya Twanga Pepeta ambalo limesogezwa mbele hadi Oktoba 6, mwaka huu, zitakuwa tayari kuwaburudisha mashabiki watakaohudhuria onyesho hilo.

Onyesho hilo mwanzoni lilipangwa kufanyika Septemba 29, mwaka huu lakini lilisogezwa mbele baada ya kutokea maafa ya kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere eneo la Ukara, Mwanza na Mkurugenzi wa Twanga, Asha Baraka, kuamua kusogeza mbele onyesho hilo ambalo litarindima kwenye Ukumbi wa Life Club zamani Century Cinema, Mwenge.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -