Tuesday, December 1, 2020

REKODI ZA ZIDANE MADRID

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

Madrid, Hispania

KATIKA mechi 33 za ligi tangu ameichukua klabu hiyo ya Real Madrid, akirithi mikoba ya Rafael Benitez tangu Januari mwaka huu, Zinedine Zidane amekuwa na rekodi ya aina yake.

Rais wa klabu hiyo ya Madrid, Florentino Perez, aliamua kwamba kocha huyo kutoka Ufaransa wakati alikuwa akiinoa Castilla, apewe kikosi hicho cha wakubwa mwishoni mwa msimu.

Ilikuwa ni uamuzi wa ajabu kumpa timu mtu ambaye hajawahi kufundisha timu kubwa hata mara moja, lakini safari ya Zidane imekuwa ya aina yake tangu amekabidhiwa timu hiyo.

Safari hiyo ilianzia na ushindi wa mechi 12 mfululizo ndani ya La Liga na kuifanya Los Blancos kukaribia kuipora Barcelona taji.

Katika msimu huu, Real Madrid wameendelea na kasi yao wakiongoza msimamo wa ligi, pointi sita juu ya kikosi cha kocha Luis Enrique, Barcelona na pointi tisa dhidi ya vijana wa Diego Simeone, Atletico Madrid.

Kwa ujumla kuanzia msimu uliopita hadi sasa, Zidane amekusanya pointi 86 kati ya 99, wakiangusha pointi 13 baada ya kutoka sare tano na kufungwa mechi  moja dhidi ya Atletico.

Pia Real wametingisha nyavu mara 99 wakiruhusu mabao 27.

Wakiwa na taji moja pekee ndani ya miaka nane, kunawafanya kuwa na kiu ya kunyakua taji msimu huu, huku wakipewa nafasi kubwa ya kuweza kufanya hivyo, wakiwa na Jose Mourinho benchi, walifanikiwa kufikisha pointi 100 lakini rekodi hiyo haiwatoshi na kila mmoja anataka kukomesha utawala wa Barcelona ndani ya La Liga.

Ushindi katika mchezo wa El Clasico, Jumamosi hii dhidi ya Barcelona utawafanya kuwa juu kwa zaidi ya pointi tisa na njia ya Zidane kunyakua taji kuzidi kuwa nyeupe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -