NA CHRISTOPHER MSEKENA
MWISHONI mwa wiki hii, msanii mkubwa wa muziki wa hip hop nchini Marekani, William Roberts ‘Rick Ross’, aliiweka picha ya Diamond Platnumz kwenye ukurasa wake wa Instagram, jambo lililotikisa mitandao ya kijamii.
Rick Ross ambaye ni mbia mkubwa wa mvinyo maarufu duniani ya Luc Balaire, amethibitisha kuwa Diamond Platnumz sasa ni balozi wa kimataifa wa kilevi hicho, huku akiwa ni zaidi ya rapa kutoka lebo ya The Industry ambaye ni balozi hapa Tanzania pekee.
Katika picha ambayo Rick Ross aliiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, ilimuonyesha Diamond Platnumz akiwa na chupa za mvinyo hiyo, ikiwa ni siku chache baada ya Rozay kuiweka picha ya mrembo, Huddah kutoka Kenya akiwa ni balozi wa Luc Balaire nchini humo.