Friday, October 23, 2020

RIPOTI YA SELCOM INAVYOONYESHA MAFANIKIO YA MFUMO WA KIELEKTRONIKI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA MWANDISHI WETU

TANGU Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilipoamua kutumia kadi za kielektroniki kuingia uwanjani, imedaiwa kuwa na mafanikio makubwa kwa mujibu wa Kampuni ya Selcom Tanzania ambayo inasimamia mfumo huo.

Mafanikio hayo yanatokana na jaribio la kwanza lililofanyika Okotaba mosi mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo iliandaliwa na Selcom na kupelekwa serikalini, TFF na klabu za soka zinazoshiriki Ligi Kuu ya Soka nchini (VPL), imeonyesha kuwa na mafanikio makubwa.

Jaribio hilo la kwanza la tiketi hizo za kielektroniki lililofanyika wakati wa mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga, inaonekana mashabiki 44,291 waliingia kwenye mchezo huo na kukusanya shilingi

354,397,000 (milioni 354.3).

Ripoti hiyo inaonyesha mashabiki walioingia jukwaa la VIP B na C ni 2762, waliongia VIP A 498 na walioingia kwenye majukwaa mengine ya mzunguko walikua 41,031.

Jumla ya kadi 168, 000 zimesambazwa na kusajiliwa kwa mashabiki ili kutumika kwa ajili ya kuingia uwanjani kwenye mechi kwa kugusisha kadi hizo kwenye mashine maalumu getini.

Kutokana na mfumo huo imedaiwa udhibiti wa wanaoingia uwanjani bila kulipa umefika asilimia 99.99.

Bado kuna mashabiki wengine wachache wanaohitaji elimu ya kutosha kuhusiana na utaratibu huo wa kadi na ndio maana Selcom ina mpango wa kutoa elimu

kupitia mawakala wake.

Mambo yanaweza yakawa mazuri zaidi kama ushirikiano wa karibu kati ya Selcom, TFF, sekta mbalimbali za Serikali na wadau wote utaendelea.

Navyo vyombo vya ulinzi na usalama vinahitajika kuhakikisha kunakuwapo na usalama wa kutosha, hasa kwenye zoezi zima la kuingia uwanjani kwa kupanga foleni.

Akizungumzia namna ambavyo wanaendelea kufanikisha jaribio hilo la awali, Meneja Miradi wa

Selcom, Gallus Runyeta, anasema uuzwaji wa kadi ulichukua wiki moja, hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa watumiaji na kusimamia kila kituo

ili kusiwapo na udanganyifu.

Lakini katika kila mafanikio hakukosi changamoto mbalimbali na Selcom wamejifunza katika hilo, ambapo moja ya changamoto hizo ni namna ya mashabiki kuingia uwanjani na kuhakiki tiketi.

Selcom imekuwa mstari wa mbele katika kuchukua ushauri wa maboresho ya mfumo huo kutokana na matumizi ya kila siku.

Hivyo Selcom imefanya maboresho katika sehemu kadhaa, imepunguza muda wa mashine unaotumika wakati kadi ya kielektroniki inapotumika, ambapo mwanzoni ilikuwa sekunde mbili hadi nusu sekunde, ili kutoa nafasi kwa mashabiki wengi zaidi kuingia uwanjani kwa muda mfupi.

Imeweka timu ya wataalamu wa kutosha uwanjani, ambao wanatoa ufumbuzi kwa changamoto zozote za kiufundi zinazojitokeza uwanjani.

“Timu hii ina simu maalumu kwa ajili ya kujibu na kurekebisha matatizo yote, tumepanua wigo wa mawakala zaidi ya 5,000 Tanzania nzima na kuwapa uwezo wa kuuza tiketi moja kwa moja kwenye kadi za mashabiki kwa uharaka zaidi na kwa usalama wa kutosha.

“Tumeweka punguzo kubwa la bei ya kadi hadi kufikia Sh 1,000 kwa kadi moja, zoezi hili limejumuisha elimu kwa mashabiki kwani kadi hii huweza kutumika kila mara mtu aingiapo uwanjani,” anasema Runyeta.

Pia Selcom wameweza kuweka mashine na matangazo ili mashabiki waweze kujisajili na kununua wenyewe tiketi kwa urahisi na matokeo yake yamekuwa mazuri.

Pia Selcom imeweka utaratibu wa kutuma ujumbe

mfupi kabla ya mechi ili kuhakikisha mawasiliano ya mechi husika na kwa wakati ili kama kuna tatizo la kimfumo lipate ufumbuzi wa haraka kuepusha malalamiko kutoka kwa mashabiki.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -