Monday, October 26, 2020

RIYAMA ALLY: CHIPUKIZI WANAWEZA KUBADILISHA LADHA BONGO MOVIES

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA ESTHER GEORGE


SANAA ni ujuzi na ubunifu ambao unaweza kumfanya mtu akavutiwa na kile unachokifanya.

Kumshawishi mtu ni kazi ngumu lakini endapo utafikisha ujumbe wenye mafundisho na uhalisia wa jambo ni lazima kila mtu atapendezwa na kazi hiyo.

Kumekuwa na wasanii wengi maarufu hapa Tanzania ambao wameonyesha ubunifu na umakini mkubwa na kufika hapo walipo leo.

Lakini je, kama leo wataachana na sanaa unadhani nini kitafuata? Hakutakuwa na wasanii tena? Jibu ni hapana kwani kuna vijana ambao bado hawajapata nafasi ya kuonyesha uwezo wao lakini wanaweza.

Umefika wakati sasa ambao hakuna jinsi ni lazima sanaa ibadilike kuwa yenye ladha tofauti tofauti ili kuweza kurudisha heshima na hadhi ya tasnia kwa kuwa na sura mpya za wasanii chipukizi.

BINGWA lilipata nafasi ya kufanya mazungumzo na mmoja wa waigizaji anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu hapa Tanzania, Riyama Ally, ambaye alifunguka mengi kuhusiana na filamu kwa ujumla.

BINGWA: Riyama wewe ni mkongwe katika tasnia labda unaweza kutuelezea hali ya sasa na ya nyuma ikoje?

RIYAMA: Kiukweli hali imebadilika tofauti na miaka ya nyuma, kwa sababu sasa hivi mashabiki wameshachoka kila siku ladha na maisha yale yale, kwa hiyo unajikuta hali inakuwa ngumu sana soko linazidi kushuka kadiri siku zinavyokwenda.

BINGWA: Tasnia ya filamu imekuwa ikitawaliwa na sura zile zile kwa muda mrefu hakuna sura mpya, we unadhani kwa upande wako inasababishwa na nini?

RIYAMA: Hiyo hali ipo na inasababishwa na waandaaji wa filamu hawawapi nafasi wasanii wachanga ili na wao waonyeshe vipaji vyao, kwani wapo wenye uwezo mkubwa ambao wanaweza kuleta ladha tofauti na inayoweza kuleta chachu ya kuzidi kuongeza juhudi ili kufikia malengo ya kuinusuru tasnia ibaki katika chati yake.

BINGWA: Unahisi ni kwanini chipukizi hawapewi nafasi?

RIYAMA: Waandaaji wa filamu wanakuwa wanaangalia umaarufu wa mtu au huyu anakitu fulani kwenye jamii na badala yake wanashindwa kujua kutoa nafasi kwa chipukizi ndicho kitu pekee kitakachompa mtu nafasi ya kutengeneza mashabiki na kufika mbali kisanaa kwa kile unachofanya na kuonekana kwa jamii.

BINGWA: Chipukizi wakipewa nafasi unadhani wanaweza kuinusuru na kuinyanyua iwe kama zamani?

RIYAMA: Mimi ninavyoona kwa sababu kutakuwa na ushindani mkubwa hivyo inaweza kuleta mabadiliko, kwa mfano mimi ni mwigizaji wa siku nyingi na nina uzoefu mkubwa anapokuja chipukizi akaonyesha kiwango zaidi pale ndipo mabadiliko yanapokuja.

BINGWA: Unawashauri nini waandaaji wa filamu kuhusu kutoa nafasi kwa chipukizi?

RIYAMA: Mimi ninashauri waandaaji wa filamu angalieni vipaji ambavyo vinachipukia, kwani wengi wao wana uwezo mkubwa ambao wanaweza kuja kufanya mabadiliko katika tasnia ya filamu na tunaweza kunyanyuka tena, kwasababu filamu zina mashabiki wengi wanapenda kazi zetu ni sisi wenyewe tunawaangusha tu, inabidi sisi tubadilike jamani.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -