Tuesday, January 19, 2021

ROBO FAINALI AFCON 2017

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

*Burkina Faso vs Tunisia ni vita ya Daudi na Goliath, Senegal v Cameroon ni muziki mnene

LIBREVILLE, Gabon

HATIMAYE ni timu nane pekee zilizobaki kwenye kinyang’anyiro cha kuliwania taji la fainali za Mataifa Afrika za mwaka huu (Afcon 2017).

Timu hizo ni Burkina Faso, Tunisia, Senegal, Cameroon, DR Congo, Ghana, Misri, na Morocco.

Moja kati ya hizo ndiyo itakayoweza kuibuka mshindi katika mchezo wa fainali utakaopigwa Februari 5.

Mbali na mechi nyingine za hatua ya robo fainali zitakazopigwa kesho, leo kutakuwa na michezo miwili inayotarajiwa kutikisa Bara la Afrika na ulimwenguni kote.

Burkina Faso watavaana na Tunisia, mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Stade de Franceville.

Lakini pia, tiketi ya Senegal kucheza nusu fainali ya Afcon 2017 itakuwa imeshikiliwa na Cameroon.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo kabla ya mchezo wa leo, Burkina Faso imecheza mechi tano dhidi ya Tunisia.

Katika idadi hiyo ya mechi, Burkina Faso wameshinda mara mbili, Tunisia wameambulia ushindi mara moja na matokeo ya sare yaliamua mechi zilizobaki.

Kwa rekodi hiyo, huenda mashabiki wa soka wasitarajie kile walichokitegemea kuwa Burkina Faso ni ‘uchochoro’ kwa Tunisia kuingia nusu fainali.

Rekodi zinaonesha kuwa Burkina Faso na Tunisia zilianza kuvaana Oktoba 22, 1995. Katika mechi hiyo ya kirafiki, matokeoa yalikuwa ni sare ya mabao 2-2.

Mchezo wa mwisho kuzikutanisha timu hizo ulikuwa wa kuwania tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2010 zilizofanyika nchini Afrika Kusini.

Mchezo huo ulichezwa Septemba 2008 na timu hizo zilimaliza dakika 90 bila kufungana.

Katika mtanange wa leo, Burkina Faso watakuwa wakimtegemea staa wa Chelsea ambaye amekuwa akipelekwa kwa mkopo katika klabu kadhaa barani Ulaya, Bertrand Traore.

Lakini pia safu yake ya kiungo itakuwa chini ya umakini mkubwa wa Charles Kabore.

Tunisia itakuwa uwanjani ikijivunia makali ya staa wao Wahbi Khazri anayekipiga Ligi Kuu England katika klabu ya Sunderland.

Nani atakayeibuka kidedea usiku wa leo kwenye Uwanja wa Stade de Franceville na kufanikiwa kutinga nusu fainali?

Mchezo mwingine unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa kandanda barani Afrika na ulimwenguni kote ni ule utakaozikutanisha Cameroon na Senegal.

Rekodi ziko wazi kuwa wababe hao wa soka la Afrika wamekutana mara 12. Senegal wameibuka na ushindi mara tano, Cameroon wameshinda tatu, na mechi zilizobaki wametoa sare.

Kwa mara ya kwanza, mechi ya kwanza kuwakutanisha wababe hao ni ile iliyochezwa mwaka 1963.

Mchezo huo uliokuwa wa michuano mnaalumu ya mataifa yaliyotawaliwa na Wafaransa na matokeo yake yalikuwa ni Senegal kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kwa mara ya mwisho, Senegal walikutana na Cameroon mwaka Juni 4, 2011. Timu ghizo hazikufungana katika mchezo huo wa fainali za mataifa Afrika.

Mashabiki wa Senegal watakuwa wakiwategemea zaidi winga Balde Keita anayekipiga Lazio ya Italia, Sadio Mane wa Liverpool, na Mame Biram Diouf anayeichezea Stoke City.

Cameroon hawaonekani kuwa na mastaa wengi kikosini lakini iambni kubwa ya mashabiki wake iko kwa nahodha Benjamin Moukandjo anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya FC Lorient ya Ligi Kuu nchini Ufaransa.

Lakini pia, winga wa kulia, Christian Bassogog,  anayecheza Denmark amekuwa msaada mkubwa kwa kikosi hicho.

Kesho michezo mingine ya robo fainali itaendelea, ambapo DR Congo Watakluwa wakimenyana na Ghana kwenye Uwanja wa Stade d’Oyem.

Siku hiyo pia, mahasimu wa Kaskazini mwa Bara la Afrika, Misri na Algeria, watakuwa wakitoana jasho kuwania nafasi ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo ya Afcon 2017.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -