Saturday, November 28, 2020

ROMA AMWAGA MBOGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA BEATRICE KAIZA,

WASANII wa Bongo Fleva, Roma Mkatoliki, Moni Central Zone, Bin Laden na kijana wa kazi, Emma Mtunya, wamesema bado hawana uhakika wa usalama wa maisha yao.

Wasanii hao walitekwa na watu wasiojulikana Jumatano iliyopita wakiwa kwenye studio za Tongwe Record zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam na kupatikana siku ya Jumamosi maeneo ya Ununio, Bahari Beach usiku wa manane.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’, alieleza jinsi walivyotekwa akisema wakati wanafanya shughuli zao za kila siku ndani ya studio za Tongwe Record, walifika watu ambao hakuweza kuwafahamu huku wakiwa na silaha za moto na jambo lao la kwanza waliwaamrisha kutoka studio na kuwataka waingie ndani ya gari.

“Tuliamrishwa kuinama ndani ya gari bila kuinuka tukiwa tumezibwa usoni kwa vitambaa na tukanza kuondoka na kwenda kuwekwa sehemu ambayo tulikaa kwa siku tatu. Tulifanyiwa mahojiano ambayo tayari nimeshaandika maelezo yake na vyombo vya dola wanaendelea na upelelezi, wakimaliza upelelezi, wao wenyewe watatoa taarifa.

“Pamoja na mahojiano hayo, tulipigwa na mimi nimeumizwa vizi za meno ya mbele,” alisema Roma akionyesha majeraha yake sehemu mbalimbali za mwili wake.

“Ijumaa usiku tukiwa tumefungwa vitambaa tena usoni, tulipandishwa kwenye gari na kuondoka bila kujua tunakoelekea kabla ya kutupwa katika dimbwi la maji.

“Nilijifungua kitambaa usoni na kuwasaidia wenzangu na kuanza kuondoka bila ya kujua tuko maeneo gani hadi tulipokutana na kibao cha Bahari Beach ndio tuligundua kwamba kule ni Ununio.

“Tulitembea kwa umbali mrefu mpaka tulipokutana na watu wa pikipiki na kurejea nyumbani kwangu Mbezi, ambapo nilifika na wenzangu na kuamua kuvunja mlango baada ya kukuta familia yangu haipo.

“Tulibadili nguo na kuondoka eneo hilo kwa kuwa tuliingia woga, tuliondoka na njiani tuliomba simu kwa dereva na kumpigia simu J-Murder (mmiliki wa studio za Tongwe Record), mwanzoni hakuamini ila tukakutana naye na kwenda kituo cha polisi,” alisema Roma.

Kwa upande wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema tukio la kutekwa kwa Roma na wenzake watatu limewashtua.

Na kuongeza kwamba kwa sasa anachosubiri ni majibu ya upelelezi ulioanza na kwamba atahakikisha anaupata na kuusema bungeni wakati anawasilisha bajeti yake.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=TWgrN-XPMD0[/embedyt]

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -