Thursday, December 3, 2020

RONALDO ALIVYOFIKISHA MABAO 500

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

YOKOHAMA, Japan

MWANAMUME! Hivi ndivyo unavyoweza kumuita straika, Cristiano Ronaldo, baada ya  juzi kufikisha  bao lake la  500 akizichezea klabu, alipofunga  bao  la pili wakati Real Madrid ikipata  ushindi wa mabao  2-0 dhidi ya Club America  katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa klabu.

Bao hilo pia ndilo lililoisaidia timu yake kutinga hatua ya fainali ya nichuano hiyo inayoendelea nchini Japan na kumfanya kinara huyo mwenye umri wa miaka 31 apige hatua kubwa katika safari yake ya kuzifumania nyavu.

Kutokana na hali hiyo, wiki hii inaonekana kuwa nzuri kwa Mreno huyo ambaye Jumatatu  alitangazwa kuwa nshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia 2016, Ballon d’Or.

Bao hilo lililopatikana kwa jitihada zake binafsi dakika ya  92 za mtanange huo uliopigwa kwenye Uwanja wa  Yokohama, ni la  39 katika mwaka huu  2016, na inavyoonekana anaweza kufunga mengi zaidi kama alivyofunga 59 mwaka 2013, kutokana na kuwa bado kuna muda mwingi.

Bao hilo dhidi ya timu hiyo kutoka Mexico ni la  377 kuifungia Real Madrid, likiwa pia limeongeza kwa yale  118  aliyofunga akiwa na  Manchester United  na matano aliyotupia akiwa na Sporting.

Mabao pia ameyafunga katika mashindano takribani  11 na huku nusu yake yakipatikana kwenye  La Liga, ambako ameshaziona nyavu mara 270.

Kutokana na idadi hiyo, winga huyo atakuwa amepiga hatua kubwa mno katika medani ya soka kutokana na kuwa alianza kusuasua katika msimu wake wa kwanza tangu aanze soka la kulipwa ambapo aliweza kufunga mabao 12 katika kipindi cha misimu mitatu kati ya mwaka  2002  na  2004.

*Timu zinazomkumbuka

Hata hivyo, kuna timu ambazo zinamkumbuka zaidi nyota huyo ambazo ni Sevilla, ambapo ameweza kuitungua mara 22 katika mechi 15 alizokutana na klabu hiyo ya Andalusia na Getafe, ambayo ameshaiumiza mara  20 katika mechi 12.

Nchini  England, mashabiki wa  Aston Villa hawana hamu na nyota huyo anayevalia jezi namba 7, kwani nao walikutana na makali ya staa huyo kwa kuchapwa mabao tisa katika mechi 14.

Kutokana na kuwa straika huyo anadai kwamba anaweza kucheza soka hadi atakapofikisha miaka  41, hakuna wasiwasi kwamba atashindwa kufikisha mabao 1,000.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -