Monday, October 26, 2020

RONALDO AMSHUKURU CUADRADO KWA KUMWACHIA JEZI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

ROMA, Italia


STRAIKA Cristiano Ronaldo amemshukuru staa mwenzake, Juan Cuadrado, kwa kukubali kumwachia jezi yake ambayo alikuwa akiitumia katika klabu ya Juventus.

Ronaldo alikamilisha usajili wake wa kujiunga na vinara hao wa Ligi ya Serie A mwezi uliopita kwa ada inayoripotiwa kuwa ni Euro milioni 112, akiwa na rekodi ya  mafanikio ambayo aliyapata akiwa na timu za Manchester United, Real Madrid na ya Taifa ya Ureno, huku akiwa na jezi hiyo namba saba mgongoni.

Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa Ballon d’Or anafahamika kwa bidhaa zake zenye nembo ya “CR7” na winga huyo wa timu ya Taifa ya Colombia hakusita kumkabidhi jezi hiyo.

“Bila shaka ni namba yangu ninayoipenda,” Ronaldo aliuambia mtandao wa DAZN.

“Kwanza nilizungumza na klabu na kisha nikazungumza na Cuadrado kwa sababu ndiye alikuwa na jezi namba saba. Nilishangaa kwa njia nzuri ambavyo klabu ilinisaidia na kisha Cuadrado akakubali bila shida. Kwa ujumla najivunia kuendelea na namba yangu saba,” aliongeza staa huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -